Advertisements

Wednesday, January 8, 2020

Hifadhi ya mafuta ya Lake Oil Dar es Salaam yateketea

By Muyonga Jumanne, Mwananchi mjumanne@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Moto mkubwa umezuka usiku wa leo Jumatano Januari 8, 2020 katika hifadhi ya mafuta inayomilikiwa na kampuni ya Lake Oil iliyoko eneo la Vijibweni Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesema wapo eneo la tukio katika jitihada za kuzima moto huo unaowaka kwa kasi.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu, Kamanda wa Polisi Temeke, Amon Kakwale amesema moto bado unaendelea kuwaka na wanashirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuhakikisha hakuna madhara makubwa yatakayotokea.

“Sisi tupo hapa kama unavyojua wananchi wengi wanapenda kuona kwa macho matukio kama haya yakitokea kwahiyo tunasimamia usalama watu wasifike eneo la tukio,” amesema Kakwale

Kakwale ameeleza wanafanya jitahada kuhakikisha malori mbalimbali ambayo hakutaja idadi yake kutokana na uwingi yanatolewa ndani ya eneo hilo ili kudhibiti maeneo yanayowaka moto.

“Hakuna taarifa zaidi ya madhara ukiacha kuungua kwa matanki ila kwakuwa tupo hapa tutaendelea kutoa taarifa zaidi,” amesema Kakwale

No comments: