Advertisements

Saturday, January 11, 2020

RAIS MHE.DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MAKAO MAKUU YA TISS - ZANZIBAR.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la jengo la Idara ya Usalama wa Taifa eneo la Maisala Zanzibar leo baada ya kupokelewa Uwanja wa Kimataifa wa Zanzibar na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Alli Iddi na Viongozi wengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika sherehe ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi Jengo la Makao Makuu ya Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) - Zanzibar. Januari 10, 2020 kuelekea sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar itakayofanyika Januari 12, 2020.
Muonekano wa ujenzi wa jengo jipya la Makao makuu ya Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) Zanzibar ukiendelea ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi Jengo hilo Januari 10,2020, kuelekea sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar itakayofanyika Januari 12, 2020. (PICHA NA IKULU

No comments: