ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 8, 2020

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MIRADI YA UJENZI YA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI, ZIMAMOTO NA UHAMIAJI, JIJINI DODOMA, LEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI UNAOENDELEA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kushoto), akiliangalia Jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji linalojengwa Jijini Dodoma, wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo, leo. Watatu kushoto ni Kamishna wa Uhamiaji, Utawala na Fedha, Edward Chogero. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (wapili kulia), akimuuliza swali Kamishna wa Utawala na Fedha, wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mbaraka Semwanza (wapili kushoto), wakati alipokua anakagua ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dodoma, leo. Kadio alifanya ziara ya kukagua ujenzi wa majengo ya Jeshi la Polisi, Uhamiaji na Ziamamoto. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kushoto), akiliangalia Jengo linalokarabatiwa la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa jengo hilo, jijini Dodoma, leo. Watatu kushoto ni Kamishna wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Jeshi hilo, Benedick Wakulyamba. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kushoto), akisalimiana na Kamishna wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Jeshi la Polisi, Benedick Wakulyamba, wakati alipokuwa anawasili Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dodoma, leo, kwa ajili ya kukagua ujenzi unaoendelea jijini humo. Kulia ni Msimamizi wa Jengo hilo, Naibu Kamishna wa Polisi, Richard Malika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kushoto), akielekea kulikagua Jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaloendelea kujengwa, jijini Dodoma. Kadio alifanya ziara ya kukagua ujenzi wa majengo yanayoendelea kujengwa ya Jeshi la Polisi, Uhamiaji na Ziamamoto, jijini humo, leo. Wapili kushoto ni Kamishna wa Utawala na Fedha, wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mbaraka Semwanza. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments: