ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 6, 2020

BOT YATOA KANUNI MPYA ZA KUWALINDA WAKOPAJI KATIKA MABENKI

Meneja Msaidizi Dawati la Malalamiko ya Wateja na Mabenki na Taasisi za Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Bw. Ganga Ben Mlipano akifafanua zaidi kuhusu mada ailiyoitoa iliyohusu Dawati hilo na namna linavyofanya kazi katika semina ya waandishi wa habari za Uchumi na Fedha kutoka vyombo mbalimbali vya habari inayoendelea kwenye tawi la BoT jijini Arusha.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Msaidizi Dawati la Malalamiko ya Wateja na Mabenki na Taasisi za Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Bw. Ganga Ben Mlipano akitoa mada kuhusu Dawati hilo na namna linavyofanya kazi katika semina ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari inayoendelea kwenye tawi la BoT jijini Arusha.
Bi. Zalia Mbeo, Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, akizungumza na wanasemina kuelezea malengo ya BoT kutoa elimu ya masuala ya Uchumi na Fedha kwa wanahabari ili kuwajengea uwezo wa kufahamu shughuli mbalimbali za Benki Kuu Tanzania.
Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, Bi. Zalia Mbeo,akizungumza na wanasemina kuelezea malengo ya BoT kutoa elimu ya masuala ya Uchumi na Fedha kwa wanahabari
Afisa Uendeshaji wa Mifuko ya Udhamini ya BoT,Bi.Kashinje Sekule Felician akiwasilisha mada kuhusu Mifuko hiyo Machi 5, 2020.
Afisa Uhusiano Mkuu Mwandamizi, Be.Lwaga Mwambande, akizungumza na wanasemina.
Kutoka kushoto kwenda kulia, Bi. Vicky Msina, Meneja Msaidizi Uhusiano na Itifaki (BoT), Bi.Kashinje Sekule Felician, Afisa Uendeshaji wa Mifuko ya Udhamini ya BoT, Bi. Zalia Mbeo, Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, Bw. Ganga Ben Mlipao, Meneja Msaidizi, Dawati la Kutatua Malalamiko ya wateja wa mabenki na taasisi za fedha, BoT na Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki, BoT Bw. Augustino Hotey, wakiwa kwenye semina hiyo.
Meneja Msaidizi Uhusiano na Itifaki BoT,Bi. Vicky Msina, akielezea uzoefu wake kwa washiriki jinsi alivyokuwa akifanya kazi za uandishi wa habari.
Bi. Zalia Mbeo, Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, akizungumza na wanasemina kuelezea malengo ya BoT kutoa elimu ya masuala ya Uchumi na Fedha kwa wanahabari ili kuwajengea uwezo wa kufahamu shughuli mbalimbali za Benki Kuu Tanzania.
BENKI kuu ya Tanzania (BOT) imeanzisha kanuni mpya (Bank of Tanzania Financial consumer Regulations) za kumsaidia mteja pindi apatapo mkopo kutoka benki mbalimbali ili kuweza kulinda haki ya hati aliyotumia kuomba mkopo huo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Arusha katika semina inayotolewa na Benki kuu ya Tanzania kwa Waandishi wa Habari za Uchumi na Fedha,Meneja Msaidizi Dawati la Kutatua Migogoro Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Ganga Mlipano amesema kuwa kanuni hizo zimetolewa
Novemba 22 mwaka 2019 na zimeeleza kuwa kila Benki itatakiwa Kuhakikisha kwamba mteja akimaliza kulipa mkopo wake ndani ya siku 30 ihakikishe imemrudishia hati aliyoitoa kama dhamana.
Pia amesema kuwa Sheria hizo zinaeleza kuwa mabenki yote ndani ya siku saba ikiwa mteja amenyimwa mkopo lazima aelezwe kwanini amenyimwa mkopo na sio mteja kusumbuka kufuatilia kwenye benki hizo kwa muda mrefu.
"kanuni hizo zinaeleza kuwa ikiwa mteja akitaka kupata mkopo lazima Benki imweleze kuhusiana na mkopo huo pamoja na athari zake",alisema Mlipano.
Amesema taratibu mbalimbali za kutatua malalamiko lazima zifuatwe na iwapo mteja amepeleka malalamiko yake benki na hayajatatuliwa, yakiletwa benki kuu kwenye dawati yatatatuliwa kwa wakati huku muda mrefu zaidi wa utatuzi ikiwa ni siku 45 pekee.
Benki kuu ya Tanzania (BOT) ilianzisha dawati la kutatua migogoro la kibenki Aprili Mosi mwaka 2015 na wamekua wakipokea na kutatua migogoro mbalimbali licha ya kukutana na changamoto mbalimbali ikiwemo wateja kukutana na mikataba yenye lugha ngumu kwa mabenki pindi wanapoenda kuomba mikopo pamoja na wateja kutopata mikopo bila kuelezwa sababu, jambo lililosababisha kuundwa kwa Sheria mpya za kumlinda mteja.

No comments: