ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 12, 2020

Mtanzania Agundulika na Virusi vya Corona

WIZARA ya Afya ya Falme za Kiarabu (U.A.E) imethibitisha kwamba raia mmoja wa Tanzania ni miongoni mwa watu 15 wapya waliokutwa na virusi vya Corona.

Watu hao 15 wenye maambukizi mapya ni Mtanzania mmoja, Afrika Kusini (1), Iran (1), Mjerumani mmoja, Italia (3), U.A.E (2), Sri Lanka (2), Uingereza (2) na India (2).

Tayari watu hao wameshawekwa chini ya uangalizi maalum na wanaendelea vizuri ambapo inaripotiwa baadhi yao waliambukizwa na wagonjwa wengine waliotoka nje ya nchi na hakuna taarifa zaidi yakiwemo majina yao.

Mpaka jana Machi 10 kuna wagonjwa wa Corona zaidi ya 140,014, vifo zaidi ya 4,000 na sasa Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema idadi ya wanaopona inazidi asilimia 70

No comments: