ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 11, 2020

Mtu wa pili apona virusi vya HIV

Paris. Mwanaume mmoja kutoka mjini London nchini Uingereza amethithitishwa kupona virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi.

Taarifa iliyotolewa na madaktari wa nchi hiyo ilisema mtu huyo anakuwa wa pili kuthibitishwa kupona ugonjwa huo.

Adam Castillejo hajapatikana na virusi baada ya kukaa miezi 30 bila kumeza dawa za kupunguza makali ya virusi vya HIV zinazofahamika kama anti-retroviral.

Castillejo ambaye sasa ana umri wa miaka 40 amejitambulisha mwenyewe kuwa hana tena virusi vya HIV baada ya mwaka mmoja kupita.

Machi, 2019 wanasayansi wa Uingereza walitangaza kuwapo kwa mgonjwa wa pili aliyepona virusi vya HIV ingawa mwathirika huyo hakujitokeza hadharani.

Mwaka 2011, Timothy Brown, mgonjwa aliyetokea katika jiji la Berlin alikua ni mtu wa kwanza kuripotiwa kuwa amepona HIV baada ya kupata tiba sawa na hiyo.

No comments: