ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 4, 2020

RC HAPI:SHULE ZOTE MKOANI IRINGA ZIJENGA CHUMBA CHA HUDUMA YA KWANZA

Mkuu wa mka wa Iringa Ally Hapi akiwa katika shule ya sekondari ya Ifunda Girls mkoani Iringa wakati wa ziara ya Iringa mpya awamu ya pili alipokuwa akikagua miradi ya elimu na kutoa tamkoa la kila shule kuwa na chumba cha huduma ya kwanza
Mkuu wa mka wa Iringa Ally Hapi,mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela  na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Robert Masunya walipokuwa wanawasili katika shule ya sekondari ya Isimila kwa ajili ya kukagua miradi ya elimuna na kutoa tamkoa la kila shule kuwa na chumba cha huduma ya kwanza
Wanafunzi wa shule ya sekondari Isimani wakimusikiliza Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi alipokuwa anatoa tamkoa la kila shule kuwa na chumba cha huduma ya kwanza

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi ameziagiza halmashauri zote kuhakikisha zinajenga chumba cha huduma ya kwanza kwenye kila shule ya sekondari kwa lengo la kuhudumia wanafunzi wanaougua ghafla au wanaohitaji kupata huduma ya kwanza katika shule hiyo.

Hayo ameyazungumza wakati wa ziara ya Iringa mpya awamu ya pili alipokuwa katika shule ya sekondari ya Isimila alipokuwa anakagua majengo ya shule hiyo na kubaini kuwa ni moja kati shule zenye chumba cha kutolea huduma ya kwanza kwa wanafunzi na watumishi wa shule hiyo.

Alisema kuwa kuna shule ambao zipo mbali na huduma ya afya hivyo wanapaswa kusafiri kwa umbali mrefu,kuwepo kwa chuma hicho kusaidia kutoa huduma majira yote ya usiku,mchana na asubuhi.

“Nimeona shule nyingi hakuna magari ya wagonjwa wala chuma cha huduma ya kwanza hivyo naagiza halmashauri zote kuhakikisha wanapojenga majengo ya shule lazima wahakikishe wanajenga au wanatenga chumba maalumu kwa ajili huduma ya kwanza” alisema Hapi

Hapi aliagiza halmashauri zote kuhakikisha kuwa wanapojenga madarasa ya  shule katikati yake lazima ijengwe ofisi ya walimu kwa lengo la kuhakikisha walimu wanapata ofisi za kuwarahisishia kazi wawapo shuleni hapo.

Aidha mkuu wa mkoa aliagiza wakurugenzi wote kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofaulu wanaendelea na masomo na kuwakamata wazazi wote ambao hawataki kuwapeleka wanafunzi shule kwa kuwa serikali inatoa huduma bure kuanzia shule ya msingi na sekondari.

“Nataka mhakikishe wanafunzi wote waliofaulu wanaenda shuleni kwa kufanya uchunguzi maalumu,serikali inarusu mwanafunzi kuanza kusoma hata akiwa anadela,suruali ambayo sio sare kwa kuwa serikali inalipa kila kitu kwa wanafunzi wote” alisema Hapi

Kwa uapnde wake mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa uwepo wa madarasa na mabweni kunachangia kuleta maendeleo ya mwanafunzi kwa kuongeza ufaulu wa masomo yao hasa wanafunzi wa kike.

“Mheshimiwa mkuu wa mkoa toka tumejenga madarasa haya mapya na mabweni kumekuwa na ongezeko za ufaulu katika hiii ya shule na shule nyingi za wilaya hii hivyo nafikiri ni jukumu letu kurudi kwa wananchi kuchangia maendeleo ya shule” alisema Kasesela

Kasesela aliongeza kuwa bado kunachangamoto ya uhaba wa majengo ya madarasa katika shule nyingi za sekondari za wilaya hiyo hivyo wananchi wanatakiwa kuendelea kuchangia matofali kwenye benki ya matofali ya kila kijiji.

No comments: