Na Zain Hamza, Washington, DC
Leo nimeona mechi tamu sana kwenye Wasafi TV. Kauzu FC walipambana na Buguruni United. Ni mechi ya ufunguzi wa mashindano kabambe ya Kivumbi cup kwa mwaka 2020.
Pongezi nyingi sana kwa walioandaa haya mashindano, vilevile pongezi nyingi sana kwa Wasafi TV kwa juhudi zao za kuonyesha mashindano hayo kwenye TV.
Ni mashindano yanayotoa fursa kwa vijana wa Tanzania kuendeleza na kuonyesha vipaji vyao vya soka mapema wakiwa bado katika umri mdogo.
Ingekuwa jambo jema kwa uongozi wa soka Tanzania TFF, kufanya juhudi za kuhakikisha mashindano ya namna hii yanafanyika nchi nzima. Vilevile wafikirie na kurudisha Taifa cup. Kama ilivyokuwa enzi zile mikoa ilipokuwa ikichuana kila mwaka kutafuta mkoa bingwa wa soka nchini kila mwaka.
Soka la Tanzania haliwezi kukua kwa kutegemea Simba na Yanga zenye wachezaji wa nchi za nje.
Katika nchi zilizoendelea kisoka duniani kama Ujerumani, Uingereza, Spain, Brazil, Argentina, Italy na kadhalika soka linalochezwa katika ngazi za chini ni kubwa mno. Uingereza ligi yao ina ngazi zaidi ya nne.
Si vibaya kwa timu kubwa kuwa na wachezaji wa nje, lakini kuwe na udhibiti fulani. Wachezaji wa Kivumbi cup waje kupata nafasi ya kuchezea timu kubwa za daraja la kwanza. Sio tija kwa wachezaji 1000 wa Kivumbi Cup watano tu ndio waje kuchezea Simba na Yanga, tena pengine wawe rizevu, kwa sababu timu hizo zimejaza wachezaji kutoka Rwanda, Burundi, Congo, Uganda, Zambia nk.
Spain wana utaratibu fulani wa kuzuia timu zao kusajili zaidi ya wachezaji watano kutoka katika nchi zisizo za umoja wa Ulaya. Ni utaratibu unaoweza kufanyiwa marekebisho kwa Tanzania ikimaanisha timu za Tanzania zisisajili zaidi ya wachezaji watano wasio watanzania.
Kwa kufanya hivyo timu za Tanzania zitakuwa na pesa za kutosha za kununua wachezaji wachache wa nje, na zitahakikisha hao wachezaji wachache wa kigeni zinaowasajili ni wa kiwango cha juu sana.
Wachezaji hao wachache wa kiwango cha juu wakiungana na wachezaji wengi wa Kivumbi cup mambo yatakuwa yatakwenda vizuri na Tanzania itarudi enzi zile za ubora wa kina King Kibaden na Sunday Manara.
Congo (DRC) na nchi za Afrika ya magharibi kama Nigeria, Senegal, Ivory Coast, Ghana, Algeria wana timu nzuri za taifa kwa sababu wana wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa Ulaya. Wamefanikiwa kufanya hivyo kwa sababu timu zao za nyumbani zinatumia zaidi vipaji vya nyumbani. Ile timu ya AS Vita iliyoiking’uta Simba bao tano ilikuwa na wachezaji wa kizaire. Lakini inasemekana ilikuwa na wachezaji watatu tu wanaochezea timu ya taifa ya DRC. Kwa sababu DRC ina wachezaji wengi wanaocheza soka Ulaya.
Sasa tunafikiaje kuwa na wachezaji wengi wanaocheza nje? Tutawapata kwa timu zetu kubwa kujaza wachezaji wa nchi za jirani? La hasha, inabidi wachezaji wa Kivumbi cup wachezee Simba na Yanga ili wakitoka nje ya nchi na timu zao waonekane kimataifa.
Ukiniuliza mimi nitakuambia Uingereza ina timu ya taifa mbaya na haijashinda kikombe chochote kwa miaka kadhaa kwa sababu ligi yao imejaa wachezaji wengi wa nchi za nje.
Hizi ni salaam, wafikishiwe TFF katika kuendeleza soka Tanzania.

No comments:
Post a Comment