Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza na waandishi wa habari
wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga wakiwa kwenye maandamano kuelekea viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga wakiwa kwenye maandamano kuelekea viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga wakiwa kwenye maandamano kuelekea viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga Specioza Owure akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa mamlaka hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
NA MWANDISHI WETU, TANGA
WANAWAKE Mkoani Tanga wametakiwa kuchangimkia fursa ya kauli mbiu ya awamu ya tano kuelekea uchumi wa viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo na vikubwa ili kuweza kujikwamua kiuchumi wao na jamii zinazowazunguka.
Hayo yalisemwa leo na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga Specioza Owure wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga.
Alisema wakina mama wasilaze damu kwa kuhakikisha wanachangamkia fursa ikiwemo kujiunga kwenye vikundi na kuanzisha viwanda ambavyo vitakuwa chachu kubwa ya kufikia mafanikio na kuweza kuwainua kiuchumi.
“Wakina mama tunaweza kufanya hivyo kwani tuna vikundi vidogo vidogo tunavyoweza kujipatia fedha ikiwemo vikoba tutumie fursa hiyo kwa kuunganisha nguvu za pamoja kufikia malengo yetu”Alisema Meneja huyo.
“Lakini pia tuhakikishe wanawake tunalipa kodi kwa hiari kwani ndio jambo muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu pia tujikite kwenye ujasiriamali ambao utakuwa chachu kubwa “Alisema
Aidha alisema kwamba pia wakinamama wajikite kufungua viwanda kikubwa na vidogo ili kuweza kuwasaidia na kutoa ajira na hivyo kuepukana na kuwa tegemezi kwa wanaume ili uchumi wa viwanda usiwapite.
“Leo ni siku ya wanawake duniani wanawake ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya Taifa lolote lile sisi TRA tumeungana na wanawake wenzetu lakini pia niwahimize mlipe kodi kwa maendeleo ya Taifa letu”Alisema
Hata hivyo alisema katika jamii watu wanaoingaika na mambo ya kiuchumi ni wanawake kuanzia ngazi ya familia mpaka maofisini hivyo wakina mama wanamcvhango mkubwa kwa maendeleo.
“Kwenye familia mwanamke ndio Waziri wa fedha na mipango, mama kama nguzo ya familia kutengewa siku yake ni jambo muhimu sana anayefahamu vizuri umuhimu wa mama ni yule ambayo mama yake ameshamtoka”Alisema
Meneja huyo alisema jamii nzima inatambua juhudi kubwa ambazo wakina mama wanafanya na sapoti wanazofanya wakina mama ambao unaweza kuwafananisha na majembe. “Pia wakina mama wanahainagika, wakina mama ni walipa kodi wazuri wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa,wakina mama wajikite kwenye shughuli za kujenga uchumi wa nchi kwa kulipa kodi kwa hiari na wakati.
No comments:
Post a Comment