ANGALIA LIVE NEWS
Thursday, April 30, 2020
Anna Mghwira Akutwa na Virusi vya Corona
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amesema amepimwa na kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.
Alisema kuwa hajui amepata wapi na lini maambukizi hayo. Lakini amesema kuwa hana dalili zozote, lakini siku tatu zilizopita aliamua tu kupima kujua afya yake.
“Kutokana na hofu na mwingiliano wa watu kutokana na mazingira ya kazi zetu niliamua kupima na matokeo yametoka nimebainika nimeambukizwa virusi vya corona. Mimi mwenyewe sina dalili, sina homa, sikohoi na sioni chochote lakini vipimo vimeonyesha nimeambukizwa.
“Kwa hiyo hii ni dalili kwamba watu wengi tunaweza kuwa tunatembea na kudhani kwamba tupo salama kumbe hatupo salama. Hivyo kupima kwa hiari ni vizuri zaidi. Siwezi kujua nimeambukizwa lini, nimeipata lini na nimepambana nayo tangu lini. Hivyo ni vyema kupima ili kujua afya zetu,” amesema.
GPL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment