Saturday, April 11, 2020

Billnass Amvisha Pete ya Uchumba Nandy

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, William Lyimo ‘Billnass’ usiku Aprili 10, 2020 amemvalisha pete ya uchumba msanii wa Bongo Fleva Faustina Charles maarufu Nandy katika kipindi cha HOMA kinachoandaliwa na TVE

Kabla ya kumvalisha Nandy pete,Billnas alipiga magoti jambo lilionyesha Nandy kitoamini anachokiona mbele ya macho yake na machozi kuonekana kumlenga huku akiwa ameshika kipaza sauti.

Nandy na Billnass waliwahi kuwa wapenzi miaka ya nyuma na mahusiano yalikatika na baadaye Nandy kuwa na uhusiano na marehemu Ruge Mutahaba mpaka pale umauti ulipomkuta.


Hata hivyo miezi michache baada ya Ruge kufariki wawili hao wamekuwa wakionekana mara kwa mara maeneo mbalimbali lakini kila walipoulizwa kama wamerudiana walikanusha jambo hilo.

Jambo hilo lilisahaulika hasa pale walipoachia wimbo wao wa ‘Bugana’ na watu kufikiri kwamba wapo kikazi kama ambavyo mara nyingi na wao wamekuwa wakijibu wanapohojiwa na pia kuitana kaka na dada.

Billnassakiwa mbele ya Nandy amesema, “leo ni siku yangu ya kuzaliwa naamini tumekuwa pamoja muda mrefu, tumepitia vitu vingi vizuri na vibaya najua upande wako mzuri na upande wako mbaya nimechagua vyote, natamani dunia nzima ijue nakupenda, nakupenda.”

“Katika maisha yangu sijawahi kufanya kitu kikubwa kama hiki kwa hiyo leo ni siku muhimu sana ni siku ya kipekee. Naamini ndio mwanzo wa ukurasa mwingine wa maisha yangu kwa hiyo ambacho naweza kukuambia nazidi kukuombea usiwe mzuri tu kwangu bali kwa mama na watoto wangu.”

chanzo GPL

No comments: