ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 6, 2020

DC IKUNGI AONGOZA MAZISHI YA DIWANI WA KATA YA KITUNTU SINGIDA

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa diwani mwenzao wa Kata ya Kituntu, Saidi Tumbwi wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo hii. 
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, akitoa salamu za rambirambi wakati wa mazishi hayo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Ally Mwanga akizungumza kwenye mazishi hayo.


Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, akizungumza kwenye mazishi hayo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Hassan Kilimba, akizungumza wakati wa mazishi hayo.
Viongozi wa chama na Serikali wa Wilaya ya Ikungi wakiwa kwenye mazishi hayo.

Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Edward Mpogolo ameongoza wananchi katika mazishi ya Diwani wa Kata ya Kitunku Saidi Tumbwi.

Tumbwi ambaye alikuwa akiumwa kwa muda mrefu amefariki usiku wa kuamukia leo na mazishi yake kufanyika leo nyumbani kwake katika kata hiyo.

Akizungumza katika mazishi hayo Mpogolo alisema wamempoteza diwani mchapa kazi na akatumia nafasi hiyo kutoa pole kwa wanafamilia, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wa wilaya hiyo kwa ujumla kwa msiba huo na kutaka kuyaenzi mambo yote ya maendeleo aliyokuwa akiyafanya Tumbwi.

Mpogolo aliwaomba wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa corona kwa kufuata maagizo yaliyotolewa na serikali ambapo pia amewaomba watanzania kuzidi kumuombea Rais John Magufuli na Taifa kwa ujumla ili kwa pamoja tuweze kuepukana na janga la corona na kuimarisha ustawi wa Tanzania yetu.

Katika salamu zake za rambirambi, Mbunge wa Singida Magharibi, Eribaliki Kingu alitoa pole kwa wafiwa, madiwani na wananchi alisema alipigania uzima wa diwani huyo kwa kugharamia matibabu lakini ndio hivyo Mungu amempenda zaidi.

Katika mazishi hayo viongozi mbalimbali wa CCM, Madiwani na Serikali walihudhuria akiwepo Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo, Mika Likapakapa, Katibu wa CCM, Noverty Kibaji, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Pius Sanka, Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Winfrida Funto na Meya wa Manispaa ya Singida, Alhaji Chima Mbua.

No comments: