ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 29, 2020

Historia Fupi ya Chief Justice Mstafu Augustino Ramadhani

Kwa masikitiko makubwa sana, tumepata taarifa ya msiba wa Kaka wa ma Kaka, Retired Chief Justice, Brigadier general, the most famous Zanzibarian Christian in Tanzanian Government History, Reverend Cannon, father, son, friend, and national hero, Augustino Ramadhani. Tunataka kutowa pole kwa mkewe, wanawe, wajuku, na family ya Ramadhani nzima. This is a monumental loss.

Kwa niaba ya familia yangu, nataka kumzunguma Justice Augustino Ramadhani kama nilivomfahamu mimi. Katika bibilia, wakristo tunaambiwa tuwe chumvi ya ulimwengu (Matayo 5:13). Kaka Augustino alikuwa chumvi iliyokolea. Justice Ramadhani ndio aliyenisogeza miye binafsi kuwa karibu na kanisa. Nimeanza kulipenda kanisa, kumtukuza mungu, na nakutaka kuwasehemu ya kushiriki katika kuendeleza ukristo visiwani Zanzibar kwa kufata mfano wake. Kabla sijamaliza form 4 (1976/1977) nilikuwa narudi kwetu bada ya kucheza mpira. Nilikutana na kijana mmoja mrefu, na mkewe mrembo, wakuvutia, na mtoto mchanga aliobebwa nyumbani kwetu (Francis). Walipoondoka nilimuliza mama, wale nani? Mama akanambiya huyu ni mkristo aliozaliwa Zanzibar aliyeishi bara miaka mingi. Ameletwa Zanzibar kikazi na anapita nyumba kwa nyumba kuwasalimiye waanglicana wenziwe na nujitambulisha.
Kama kumbukumbu zangu sahihi, Marehemu Jumbe aliyekuwa raisi wa Zanzibar alitembelea kambi ya jeshi nachingwea. Ndipo alipo kutana na Leuitenant wa jeshi moja alomwamkia raisi. Alivojitambulisha kwa Raisi, raisia akamuliza wewe ni mtoto wa Mwalim Matthew? Akasema ndio. Raisi akamuliza Justice Ramadhani, unafanya nini huku jeshini? Akamjibu, mimi ni mwana sheria. Raisi akamwambia kwamba Zanzibar tunaupungufu mkubwa wa wanasheria. Bada muda si mrefu, Justice Ramadhani akapewa barua ya transfer kutoka jeshini na kujakufanya kazi katika Serekali ya Zanzibar kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Na kwa wakati huo, mwasheria mku alikuwa Daniel Lubuva. Yeye alikuja kutoka bara pia. Kutoka hapo kaanza kazi ya kusaidia wa zanzibari katika mambo ya sheria na hajasimama.

Daniel Lubuva alimpeleka pemba kwa mda mdogo na akarudishwa Zanzibar baada ya kuweka mambo sawa pemba. Raisi alipotaka kumbadlisha Jaji mku wa Zaznibar (Marehemu Omar Borafya), Justice Augustino Ramadhani alichaguliwa kuwa Jaji mku wa Zanzibar. Aliweka historia kwa kuwa Jaji mku mdogo akiwa na miaka 34. Haijawahi kutokea Tanzania. Justice Ramadhani alianza kazi yakugeuza mahakama ya Zanzibar. Siku hizo, Ilikuwa haina utaratibu malum waki mahakama. Na kama historia ya Zanzibar itaandikwa siku moja, basi Justice Ramadhani ndiye aliorudisha Mahakama ya Zanzibar kuwa kama mahamakam za duniani kote. Kama kawaidi, mambo mengi hubadilika bada ya mapinduzi. Na mahakama ya Zanzibar ilibadilika kupita kiasi. Hata mahakama ikawa hairuhusu mshatakiwa yeyote kuwa na wakili wakumtetea. Justice Ramadhani karudisha haki za binadamu. Waziri kiuongozai (Seif Shariff Hamad) na Raisi wa Zanzibar (Marehemu Abdulwakil) walisimama naye na walikubali kwamba mabdliko hayo yanahitajika.
Aliopandika barua yakujiuzulu nafasi yake kama Jaji mkuu wa Zaznibar, alimwandikia aliyekuwa waziri wa ulinzi na jeshi lakujenga taifa Dr. Salim Ahmead Salim kumweleza kwamba Jaji Mkuu wa Zanzibar mpya atachanguliwa karibuni na yukotayari kunedelea kufanya kazi zakuendleza nchi yake nakusaidia waTanzania. Akamomba ampangiye kazi kwa sababu yeye ni mwanajeshi alokuwa na cheo cha Colonel. Mambo hayakwenda hivo. Mungu alikuwa na mpango mwengine kwake. Aliyekuwa Raisi wa Tanzania (Mwinyi) alimteua kuwa jaji katika wa mhakama ya rufaa Tanzania. Hamid Mahuoud ndiye aliye rithi nafasi ya Justice Ramadhani katika serkeali ya Zanzibar. Nalikweka history kuwa jaji peke aliofanya kazi ya jaji mku wa Zanzibar kwa kipindi cha Zaidi ya miaka 25.

The rest is history. Kutoka Court of Appeal Justice #4 Augustino Ramadhani kaendelea kuwa Chief Justice wa Nchi ya Tanzania (State of Tanzania). He’s one of us. Zanzibarian, Christian, Hard Working, and following God’s plan for his life.

Turudi katika maisha yake alivokuwa Zanzibar. Mimi nakumbukwa kwama kila asubui akienda kazini, akirudi kwake. Na kila jumanne na alhamisi akija kanisani mkunazini kufundisha choir. Na kila jumapili ya mungu, akipiga kinanda kwenye kanisi kuu. Katika misa ya shangwe. Wakati huo huo, alianzisha darasa la cheti cha sheria. Akawa mwalim anosomesha Certificate of Law wiki mara mbili kwenye shule ya tasisi ya lugha ya kigeni. Naalimwomba mwanasheria mkuu wake, Hamid Mahmoud, aje kumsaidiya kufunisha darasa hilo. Na alifanya kazi hiyo bila malipo.

Sasa tujiulize, tunaweza kujifundisha nini katika maisha ya Justice Reverand Cannon Augustino Ramadhani? Mimi nitamkumbuka rafiki wangu mpenzi hivi. Hakupenda mambo makubwa kama mafundisho ya bwana yesu yanavyotwambiya. Hakuwa na tama ya mali wala vitu vya dunia hi. Alikuwa na heshima yakupindukiya. Alihemishumu wakumbwa zake na wadogo zake. Aliona umuhimu wa elimu. Maisha yake yote alitafuta wakati wakulimarisha kanisa. Kila mmoja katika sisi anaouwezo wakuiga mfano wake. Kila mmoja wetu katika sisi akifata moja ya mambo aliyofanya Justice Ramadhani, jumuia yetu ya wa Anglicana wa Zaznibar tutaona maendeleo yasokuwa na mfano. Bwana ametowa. Bwana ametwa. Jina la bwana lihimdiwe. Rest in peace my dear friend.

Alban Abdalla

No comments: