WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema maambukizi mapya ya ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona, sasa yamefikia watu 480 ambapo wagonjwa wapya ni 196 ambapo kati yao Bara ni 174, Zanzibar 22.
Aidha, amesema kuwa idadi ya wagonjwa waliopona imeongezeka kutoka 48 hadi kufikia 167, (Zanzibar wako 36, Bara ni 83).
Hali kadhalika vifo sita vimetokea na kufanya jumla ya waliofariki kwa ugonjwa huo kufikia 16 hadi sasa.
Pia ametoa rai kwa Watanzania kuacha kutoa taarifa za uzushi za vifo na kwamba kila kifo kinachotokea ni Covid-19.
No comments:
Post a Comment