ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 29, 2020

Simba kila safu wachezaji watatu wapya

By THOBIAS SEBASTIAN

UONGOZI wa Simba umeanza kufanya mipango thabiti ya kuhakikisha kila eneo kwenye kikosi chao wanapendekeza wachezaji watatu ambapo mmoja kati yao mwenye uwezo mkubwa atasajiliwa.
Simba wameanza mchakato huo wa usajili baada ya kupokea ripoti ya awali kutoka kwa kocha wao mkuu, Mbelgiji Sven Vanderbroek ambayo wameanza kuifanyia kazi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema wamepokea ripoti ya kocha wao, siku nyingi nyuma kabla ya janga hili la ugonjwa wa Covid -19, wameanza kuifanyia kazi katika maeneo ambayo yamependekezwa.

Senzo amesema Sven, ametaka wachezaji wengi ambao wanamaliza mikataba wabakishwe ndani ya timu na usajili utakaofanyika kipindi cha usajili uwe wa kawaida usikuwa na wachezaji wengi kwani wakisajiri wapya wengi hawatakuwa na timu imara msimu ujao.

Amesema usajili wao utakuwa wa wachezaji wachache na kila eneo moja ambalo Sven anataka mchezaji mpya uongozi watakuwa na machaguo matatu ya wachezaji wapya ambapo mmoja kati ya hao ndiye atakayesajiliwa kwa kuzingatia ubora wake.

"Nadhani kipindi hiki mambo mengi yamesimama kutokana na ugonjwa huu lakini mambo yakiwa sawa kila kitu tutakifanya na kukiweka wazi, jambo ambalo lipo mbele yetu ni kufikiria namna gani ambavyo tutamaliza ligi," amesema Senzo.

No comments: