ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 6, 2020

Karibu katika juma la nne la majadiliano na uelimishaji kuhusu janga la Corona.

Karibu katika juma la nne la majadiliano na uelimishaji kuhusu janga la Corona.
Majadiliano haya yamefanyika Jumamosi ya Aprili 4, 2020
Juma hili, utasikiliza majadiliano na wataalamu wa Afya waTanzania kuhusu janga hili.
DICOTA (Baraza la waTanzania waishio nchini Marekani), ikishirikiana na TUHEDA (chama cha wadau wa afya wa asili ya Tanzania waishio UK) waliratibu majadiliano na Wataalamu wa Afya WaTZ walio mstari wa mbele kukabiliana na janga la COVID-19. Ni mjadala kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwa na uelewa mpana wa mapambano haya kwa lugha yetu toka kwa wale wanaotoka kwetu.
WATAALAM HAWA WANAZUNGUMZA KWA UELEWA, UZOEFU NA MIIKO YA KAZI LAKINI SI KAMA WASEMAJI AMA WAWAKILISHI WA SEHEMU ZAO ZA KAZI.

Watoa mada juma hili walikuwa

Dk. Ndema Habib, MSc (Biostatistics), PhD - Geneva, Switzerland

Dk. Mohamed Salim, MD, MSc, MSc (Public Health, Substance Abuse) - London, UK

Dk. Karima Khalid, MD, MMed (Anaesthesia and Critical Care) - MOI/MUHAS, Dar es Salaam, Tanzania

Dk. Harrieth Gabone-Mwalupindi, PhD, MSN, RNC (Obstetrics) - Florida, USA
Pia tulipata muendelezo wa hali ilivypo nchini Uingereza kutoka kwa Dr Gideon Mlawa.

- Muongoza mjadala ni Dr Frank Minja, toka Connecticut hapa Marekani

No comments: