ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 9, 2020

MAKATIBU WAKUU WATEMBELEA MIUNDOMBINU YA KUUKABILI UGONJWA WA CORONA DAR NA PWANI

Makatibu Wakuu wametembelea Hosteli za Magufuli, Kiwanda cha kuzalisha Barakoa, Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani na eneo ambalo linajengwa Hospitali ya Kisasa ya magonjwa ya mlipuko ambayo ipo eneo la kisoka km 1 kutoka hospitali ya Mloganzila. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu ya kukabiliana na COVID-19 baada ya kutembelea Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani leo tarehe 8 Aprili, 2020.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu ya kukabiliana na COVID-19 na wataalamu wa Afya waliopo katika Hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam maarufu Magufuli. Kamati hiyo imefanya ziara leo tarehe 8 Aprili, 2020. Hosteli za Magufuli ni moja ya maeneo waliyotembelea.
Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Zainab Chaula wakitembelea Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, ambapo jengo moja lenye vitanda 40 litatumika kuwahudumia wagonjwa watakaobainika kuwa na virusi vya Corona.
Meneja wa mradi wa ujezi wa Hospitali ya kisasa ya magonjwa ya mlipuko, Kanali Solomoni Chausi akitoa taarifa mbele ya Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu ya kukabiliana na COVID-19 walipofanya ziara ya kutembelea mradi huo.
Meneja operesheni wa kiwanda cha kuzalisha barakoa cha kampuni ya Pristine kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam akitoa taarifa kuhusiana na kiwanda hicho mbele ya Kamati ya Kitaifa ya kukabiliana na COVID-19 walipotembelea kiwanda hicho leo tarehe 8 Aprili, 2020.
Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu wakiwa ndani ya kiwanda cha kampuni ya Pristine kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam kuona jinsi uzalishaji wa Barakoa unavyofanyika kwenye kiwanda hicho.

No comments: