Monday, April 20, 2020

Muhimbili Yafafanua Muuguzi Anayedaiwa Kufa kwa Corona

Kuna taarifa inasambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Evodia Kapinga amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Corona na kwamba alikua akihudumia wagonjwa wa Corona. Kapinga hajawahi kuhudumia wagonjwa wa wanaougua ugonjwa wa Corona.

Evodia alikua akitoa huduma kliniki ya watoto wenye tatizo la afya ya akili iliyopo jengo la watoto.
Evodia ni mgonjwa wa siku nyingi aliyekua akisumbuliwa na MARADHI AMBAYO HATUWEZI KUYATAJA KULINGANA NA MAADILI YA TIBA.

Jana Jumamosi tarehe 18 Aprili, 2020 saa NNE USIKU Evodia akiwa nyumbani kwake Kimara, alizidiwa ambapo watoto wake walifanya jitihada ya kumkimbiza Muhimbili lakini wakiwa njiani hali yake ilibadilika ndipo walipompeleka Hospitali ya karibu ya Sinza, Palestina.

Madaktari na Wauguzi walifanya kila jitihada kuokoa maisha yake bila mafanikio ambapo amefariki leo Jumapili saa 09 alfajiri.

Hivyo, taarifa
zinazosambaa kuwa kifo chake kinatokana na ugonjwa wa Corona siyo za kweli, ZIPUUZWE.

Imetolewa na;
Aminiel Aligaesha
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Dar es Salaam, Jumapili Aprili 19,2020

No comments: