ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 21, 2020

TUZALISHE KWA WINGI BIDHAA TULIZOKUWA TUNAAGIZA KUTOKA NJE: PROF SHEMDOE

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe wa kwanza kulia akiwa kwenye Mkutano wa Watalaam wa Mashirika ya Viwango kutoka nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya Video katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tanzania, wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.Athuman Ngenya.

Na Erick Msuya

Wazalishaji wa Bidhaa mbalimbali nchini wametakiwa kuzalisha kwa wingi bidhaa zilizokuwa zinaagizwa kutatoka Nje ya Nchi, kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa hizo kulikosababishwa na ugonjwa wa Corona, pamoja na kuitumia fursa ya uwepo wa Bandari hasa kwaajili ya kuhudumia soko la SADC.

Wito huo umetolewa Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe wakati akifungua Mkutano wa wataalam wa Mashirika ya Viwango kwa nchi za SADC uliofanyika kwa njia ya Video katika Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere JNICC.

Prof.Shemdoe amesema kutokana na kufungwa kwa baadhi ya mipaka ya Nchi na upungufu wa upokeaji wa bidhaa kutoka Nje, wakati sasa umefika kwa wazalishaji wa ndani kutumia fursa hiyo kwaajili ya kuzalisha bidhaa kwa wingi zaidi.

“Tunatatizo la Corona nchini, na baadhi ya biashara kupitia mipakani zimepungua hivyo kusababisha kupungua kwa bidhaa kwenye nchi zinazotegemea bandari zetu, hii ni fursa kwetu hivyo tuzalishe kwa wingi kwaajili ya nchi hizo ambazo zinatuzunguka na ambazo zinategemea bandari zetu” alisema Prof. Shemdoe

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.Athuman Ngenya (kushoto), akizungumza kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe kufungua Mkutano wa Watalaam wa Mashirika ya Viwango kutoka nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya Video katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tanzania.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe wa kushoto akifungua Mkutano wa Watalaam wa Mashirika ya Viwango kutoka nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya Video katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tanzania, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.Athuman Ngenya.


Aidha Prof. Shemdoe alisema lengo kuu la Serikali ya Tanzania ni kuzalisha kwa wingi Viwandani bidhaa zenye ubora na zenye uwezo wa kushindana katika masoko ya nchi za za SADC na Kimataifa ili kuweza kufikia malengo makuu ya kupambana kiuchumi hasa katika kipindi hiki ambacho maradhi ya Corona yameenea katika nchi mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania Dkt. Yusuph Ngenya amewataka wamiliki wa Viwanda na Wazalishaji wa bidhaa kuendelea kuzalisha bidhaa zenye Ubora na Viwango ili waweze kushindana na kununuliwa kwa wingi na nchi 16 wanachama wa jumuiya ya SADC na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.Athuman Ngenya, akiendesha Mkutano wa Watalaam wa Mashirika ya Viwango kutoka nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya Video katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tanzania.


Watalaam wa Shirika la Viwango kutoka Tanzania wakiwa kwenye Mkutano wa Mashirika ya Viwango wa nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya Video katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tanzania.

“Niwaombe wenye viwanda na watengezaji wa bidhaa ndani ya nchi wajitahidi kutengeza bidhaa zenye viwango na ubora, sababu kiwango kikishapita hapa Tanzania, basi soko lote la nchi 16 za SADC bidhaa itaweza kununuliwa, hivyo ni wakati sasa wa soko kututambua ndani ya Afrika na Nje ya Afrika. Alisema Dkt. Ngenya

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.Athuman Ngenya (kulia) akiendesha Mkutano wa Watalaam wa Mashirika ya Viwango kutoka nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya Video katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tanzania, kushoto ni Watalaam wa Shirika la Viwango kutoka Tanzania wakifuatilia mkutano huo.

Watalaam wa Shirika la Viwango kutoka Tanzania wakifuatilia kwa makini Mkutano wa Mashirika ya Viwango wa nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya Video katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tanzania.

Shirika la Viwango Tanzania TBS ni miongoni mwa mashirika ya viwango yanayotambulika na kuheshimika kimataifa kwa weledi na utoaji wa viwango vya kimataifa hivyo bidhaa za ndani zitakazothibitishwa na Shirika hilo zitakuwa na ubora na viwango vya Kimataifa.

No comments: