ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 21, 2020

MAOMBI YA KITAIFA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA, WAZEE NA WATOTO


Mji wa Serikali Mtumba
Mtaa wa Afya.
S.L.P. 573.
40478 DODOMA
2
Simu Na.255-26-2963341/296334
Nukushi: 255-26-2963348 
Barua Pepe: ps@jamii.go.tz

Tovuti:www.jamii.go.tz 


TAARIFA KWA UMMA

MAOMBI YA KITAIFA DHIDI YA JANGA LA CORONA.

Dodoma, Jumanne 21 Aprili, 2020

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Viongozi wa madhehebu ya Dini nchini, imeandaa maombi maalum Kitaifa kuiombea Nchi dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayotokana na Virusi vya Corona.

Maombi hayo yatakayoongozwa na Viongozi Wakuu wa madhehebu ya Dini nchini, yatafanyika Jumatano tarehe 22 Aprili, 2020 katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar Es Salaam, kuanzia Saa 3.00 Asubuhi ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hatua hii ni utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa viongozi wa Dini na Serikali uliofanyika tarehe 9 Aprili, 2020 Jijini Dar Es Salaam kuwa yafanyike maombi ya kitaifa yanayojumuisha madhehebu yote nchini kuomba dhidi maambukizi ya Corona.

Aidha, maombi haya ni mwendelezo wa maombi ya siku tatu mfululizo yaliyotangazwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuanzia tarehe 17-19 Aprili, 2020.

Viongozi wachache watahudhuria maombi haya kuwakilisha wananchi ikiwa ni katika hali ya kuchukua tahadhari ya maambukizi hivyo, wananchi mnasisitizwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona na kufuatilia maombi haya mkiwa katika maeneo yenu kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

JIKINGE, WAKINGE WENGINE CORONA INAZUILIKA.

IMETOLEWA NA


Prudence Constantine,
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
(Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii).

No comments: