WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema, hadi Aprili 21, 2020 jumla ya wagonjwa 284 wamethibitika kuwa na #COVID19; Wagonjwa 256 wanaendelea vizuri, 7 wako kwenye uangalizi maalum, 11 wamepona na 10 wamefariki.
Mara ya mwisho Waziri wa Afya alitoa taarifa kuwa jumla ya visa vya wagonjwa wa COVID-19 ilikuwa 254 baada ya wagonjwa 84 kuongezeka.
Aidha, Waziri Mkuu amesema jumla ya watu 2,815 waliokuwa karibu na wagonjwa wamefuatiliwa afya zao ambapo kati yao, watu 1,733 hawana maambukizi na watu 12 walikutwa na virusi hivyo (wapo kwenye orodha ya watu 284).
Ameyasema hayo akiwa kwenye maombezi ya kuombea taifa dhidi ya ugonjwa huu yanayofanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar.
“Jumla ya wagonjwa 284 wamethibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona, kati ya hao wagonjwa 256 wanaendelea vizuri kiafya, wagonjwa 7 wako kwenye uangalizi wa karibu kadhalika wagonjwa 11 walishapona kabisa.
““Nimshukuru sana Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amefanya kazi kubwa, yeye na Katibu Mkuu wake, Mganga Mkuu wa Serikali, pamoja na Madaktari wetu wote, kazi mnayoifanya kama msingefanya hivyo tungekuwa kwenye hali mbaya, Watanzania wanajua unachokifanya, Mama unaweza.
“Leo nikiwa napita njiani nimewaona Watanzania wengine wamevaa ‘handkerchief’, lengo ni kuzuia kufikiwa na maambukizi, hii nayo inaweza kuzuia maambukizi.
“Serikali tumeunda kamati ya Kitaifa yenye lengo la kufuatilia mwenendo wa ugonjwa huu, tumeunda kamati ambayo itaongozwa na Waziri Mkuu, nyingine ikiongozwa na Makatibu Wakuu, tumeunda pia timu ya Madaktari waliobobea katika utafiti.
“WHO walikadiria kwamba kufikia mwisho wa mwezi Aprili, tungekuwa na wagonjwa zaidi ya laki tano, lakini kwa kadirio hilo hatujaweza kufikia, Jiji la DSM na Zanzibar ndiyo wanaoongoza kwa maambukizi ukilinganisha na Mikoa mingine,” amesema Majaliwa.
Pia, amesema Rais Magufuli na Makamu wake, Samia Suluhu wamemtuma awasilishe salamu za upendo na shukrani kwa wote wanaoonesha jitihada katika kupigania maisha ya watu wote hapa nchini.
No comments:
Post a Comment