Mkurugenzi wa CSI nchini Tanzania Stella Mpanda akizungumza na wananchi waliofika katika ofisi za shirika la kimataifa la Childbirth Survival International (CSI) kwa ajili ya kupatiwa msaada wa chakula kwenye kipindi hiki vha janga la Covid-19.
Mkurugenzi wa CSI nchini Tanzania Stella Mpanda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shirika hilo lilivyoshiriki kikamilifu kwenye ugawaji wa vyakula kwa kaya maskini kwenye kipindi hili cha janga la Ugonjwa wa Covid-19.
Mwenyekiti wa mtaa wa Mazizini kata ya Ukonga jijini Dar es Salaam Mussa Komba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna zilivyopatikana kaya maskini pamoja na walivyosimamia ugawaji wa vyakula kutoka shirika la kimataifa la Childbirth Survival International (CSI).
Mmoja ya wananchi ambaye amepata msaada huo Habiba Tawaqal akitoa shukrani kwa shirika la kimataifa la Childbirth Survival International (CSI) mara baada ya kupokea msaada wa chakuka kutoka katika shorika hilo leo jijini Dar es salaam
SHIRIKA la kimataifa la Childbirth Survival International (CSI)limetoa msaada wa vyakula , sukari na sabuni kwa kaya zaidi ya 50 za watu wasiojiweza zinazoishi Kata ya Mazizini Ukonga jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu moja wapo ya kuzisaidia kaya hizo katika kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa Covid-19.
Kwa mujibu wa CSI ni kwamba linatambua changamoto ambazo jamii ya Watanzania inapitia zikiwemo kaya masikini ambazo Corona imesababisha hata shughuli za utafutaji riziki kuwa mgumu na hivyo wameona ni vema kuzisaidia kwa kuzipatia mchele, unga, maharage, sukari na mche wa sabuni.
Akizungumza leo Mei 2 mwaka 2020 jijini Dar es Salaam wakati wa utoaji wa msaada huo, Mkurugenzi wa CSI nchini Tanzania Stella Mpanda amesema wamekuwa wakihusika za kusaidia wanawake,wajawazito na vijana lakini kwa wakati huu wa mambukizi ya Corora kupitia ofisi zao zilizoko Marekani na za hapa nchini Tanzania wameamua kuwakarimu wanananchi wasiojiweza.
"Wananchi hawa ambao hawana uwezo wamekuwa wakipata changamoto kwenye utafutaji riziki na kipindi hiki cha Corona hali zao kiuchumi ni mbaya zaidi, hivyo shirika letu limeamua kuwasaidia vyakula vya aina mbalimbali, sukari na sabuni.
"Kwa hiyo tumeona tuwasaidie kwa kiasi, kwa kuchukua hiki kidogo ambacho tunacho, kwa siku ya leo tumesaidia zaidi ya kaya 50 na wote hao tumewapa mchele, sukari maharage,unga na mche wa sabuni,hivyo ambavyo tumetoa kwetu tunaona ndio jambo la msingi. Tutaendelea kusaidia jamii yenye uhitaji kadri tutalavyojaaliwa kupitia wadau wetu mbalimbali"amesema Mpanda.
Kuhusu Corona, Mpanda amesema kuwa wametumia nafasi hiyo kuwahamasisha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ambazo zinatolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwani kumewepo na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na jamii Watanzania lazima wayafuate ili kukabiliana na ugonjwa huo hatari.
Mpanda amesema kuwa kasi ya maambukizi ya Corona kwa sasa ni kubwa, hivyo ni muhimu wananchi kuendelea kuvaa barakoa, kunawa maji tiririka na sababu , kupaka vitakasa mikono huku akisisitiza ugonjwa huo ni halisia na unaua.
"Hivyo lazima tuchukue tahadhari na kubwa zaidi tuache mikusanyiko isiyokuwa ya lazima na kama hakuna ulazima wa kutoka nyumbani basi ni vema ukakaa kwako tu, tuzingatie kuachiana nafasi tunapokaa angalau mita moja kutoka mtu mmoja hadi mwingine kama ambavyo tunaambiwa na Serikali,"amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kata ya Mazizini Ukonga jijini Dar es Salaam Mussa Komba ametoa shukrani kwa niaba ya wananchi kutokana na msaada huo huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kufuata maelekezo ambayo yanatolewa na Wizara ya Afya na kwamba ili kukabliana na ugonjwa huo kila mtu kwa nafasi yake anatakiwa kuchukua hatua ikiwemo ya kufuata maelekezo ya watalaam wa afya.
Mmoja ya wananchi ambaye amepata msaada huo Habiba Tawaqal amesema anashukuru CSI kwa kutoa msaada huo na wao wamefarijika sana kwani umekuja wakati mauafaka na kuongeza ni muhimu kwa jamii kuvaa barakoa kwani Corona ni hatari sana.
No comments:
Post a Comment