ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 3, 2020

JINSI YA KUJIEPUSHA NA MAAMBUKIZO YA CORONA KATIKA KIPINDI HIKI CHA RAMADHAN KAREEM.

1st Confirmed Case of Coronavirus in NH – NBC Boston
BY MOHAMED MATOPE

Mambo yanayowaweka waislam kwenye riski ya kuambukizwa coronavirus wanapokwenda kuswali misikitini wakati huu wa Ramadhan:

1. Ongezeko la nafasi ya maambukizo ya corona; Nguzo za dini zinatulazimu tuswali mara 5 kwa siku. Kwa maana hiyo muumini kama ataenda msikitini mara zote hizi, anakuwa na chance 5 za kuambukizwa coronavirus kila siku. Tofauti na wakristo wanaokwenda kanisani mara moja kwa wiki.

2. Waislam tunagusa nyuso zetu mara nyingi wakati wa kuchukuwa udhu , kuswali na kuomba dua . Wadudu wa coronavirus wanaingia mwilini kupitia usoni.

3. Wakati wa kuchukuwa udhu tunatumia vifaa kama kata na makopo ya kuchotea maji au mabomba ya maji, ambayo yanapitia mikono mingi ya watu bila kuwa sterilized between use. Kwa hiyo kama mtu mmoja akiacha virus kwenye kata au bomba ni rahisi kusambaa kwa watu wengine watakaoshika hizo sehemu.

4. Sheria za dini yetu hairuhusu kuvaa viatu tukiwa ndani ya misikiti. Coronavirus wanaishi kwenye nyayo. Ni rahisi kwa mtu kubeba coronavirus kwenye miguu wakati wa kuchukua udhu na kuviweka kwenye sakafu au mikeka ya kuswalia wakati anapotembea kuingia ndani ya msikiti.

5. Tunapo sujudu sura zetu zinagusa chini ya sakafu, na kuwa exposed kwa coronavirus kuingia machoni na puani.

6. Tunapomaliza swala tunapeana mikono na kisha baada ya dua tunagusa nyuso zetu .

7. Corona inatapakaa kiurahisi kwenye mikusanyiko ya watu wengi, na coronavirus wanaishi kwenye mikeka na sakafu mpaka masaa 48 (siku mbili). Kwa maana hiyo, kama mtu mmoja akiwa kaathirika , anakuwa na nafasi kubwa ya kusambaza virus kwa watu wengi.

Vitu ambavyo inabidi vitendeke misikitini ili wauumini waswali bila kuwa na riski ya kuambukizwa coronavirus.

1. Misikiti inabidi iwe na wauguzi na manesi wa kuwa screen watu wote wanaokuja kuswali, wapime homa na kuwafanyia Covid-19 questionnaire.

2. Misikiti unabidi ufanyiwe usafi wa hali ya juu (deep cleaning ) kila baada ya swala . Maana yake ni kumwagiwa dawa za kuua virus ndani ya msikiti kwenye sakafu na kuta zote mara tano kwa siku .

3. Misikiti iwe na ndoo ya disinfectant solution ambazo kila muumini alazimike kuosha na kulowesha miguu yake kabla hajaingia ndani ya msikiti.

4. Waumini wapake sanitizer mwili mzima na usoni baada ya kuchukuwa udhu, kabla hawajaingia msikitini.

Kuna tahadhari zaidi ya kumi ambazo inabidi zifuatwe misikitini ili watu waswali salama na kuepuka riski za maambukizo ya corona. Nimeorozesha tahadhari kubwa 4 za mwanzo ili kutoa picha kamili jinsi gani hizi tahadhali zilivyokuwa na gharama kubwa za utekelezaji wake, na zinavyohitaji juhudi na resources nyingi. Point yangu ni kuwa, hatuna uwezo wa kipesa,kiutaalamu na nidhamu ya kuweza kuzitekeleza hizi tahadhari.

Hii pia ni sababu moja kubwa nchi tajiri za kiislamu za gulf states, Bahrain, Kuwait, Oman, Qatar, Saudi Arabia na the United Arab Emirates, zimeamua kufunga misikiti yao yote na kuamrisha raia wao waswali majumbani. Kule Kuwait wao wenzetu wameongeza mwisho wa kila adhana- ambazo zinasikika mji mzima mara tano kwa siku - sentensi inayosema “tafadhali swali nyumbani kwako”.

Vilevile riski kama hizi ndizo zimesababisha taifa la kiislamu na chanzo cha dini yetu, Saudi Arabia, wafunge misikiti mitakatifu ya MECCA NA MADINAH. Mahali kwenye kaburi la Mtume Muhammad, sehemu inayoeleweka kama KIBRA, ambapo sura zetu zinaangalia wakati wa swala na maziko kaburini

Kwa sasa njia pekee ya maana na msingi ya kulinda usalama wa waumini kwa wakati huu wa coronavirus pandemic ni kufunga misikiti yote kwa ibada za watu wengi kwa wakati mmoja, watu waswali majumbani kwao na kufuata mila na practice zote za jadi za swala bila kujiweka kwenye risk ya kuambukizwa corona.

No comments: