ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 9, 2020

Mbunge ‘Agundua’ Dawa ya Corona, Adai 30 Wamepona

MBUNGE wa Lushoto, Shabani Shekilindi, amedai amegundua dawa inayotibu ugonjwa wa Corona, ambapo kwa sasa ameikabidhi Serikalini ili kupata uthibitisho wa maabara. Shekilindi ameeleza mpaka sasa ameshatibia wagonjwa zaidi ya 30 na wote wamepona.

Amesema: “Mimi nimekuwa na bibi zangu na babu zangu kwa hiyo hivi vitu ni kama vile nimerithishwa. Wakati ule ninakuwa na bibi na babu, tulikuwa tunakwenda msituni au porini kutafuta mizizi, kwa hiyo walikuwa wakiniambia kuwa dawa hii na hii ukiichanganya inatibu ugonjwa fulani.

“Sasa mimi mwenyewe nikajiongeza baada ya corona hii kutokea. Baada ya kujiongeza nikatest, baada ya kutest ni kweli ikawa inatibu corona. Na inatibu Corona kwa masaa 11 tu mgonjwa amepeona,” amesema.

Idadi ya alioponyesha

Kuhusu idadi ya watu walioponyeshwa, alisema, “Siyo mmoja. Ni wengi. Kesi nyingi. Ndugu ndiyo wanakuja kuthibitisha kuwa huyu amepimwa na ana virusi vya Corona. Idadi ya wagonjwa niliowaponya siwezi kujua idadi yake lakini ni wengi sana, wanafika zaidi ya 30.

Kuhusu hatua gani amechukua kushirikisha mamlaka za serikali, amesema: “Nimempigia kwanza mheshimiwa Waziri Mkuu, na Waziri Mkuu akampigia Mh. Ummy naye akanipigia, akamtumia bwana mmoja kutoka NIMR anaitwa Mgaya. Baada ya hapo Mgaya akaja kuchukuwa sample, kwa hiyo mpaka sasa hivi nasubiria tu majibu kutoka maabara kwa Mkemia Mkuu.”

Kuhusu utaratibu endapo dawa itagundulika kutibu Corona, amesema: “Serikali itaweka utaratibu wake. Siyo mimi tena.” Pia ameeleza kutakuwa na gharama kidogo ya fedha kupata huduma hiyo endapo dawa itathibitishwa kufanya kazi.

GPL

No comments: