ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 5, 2020

Tanzia: Dkt. Lamwai Afariki Dunia


Profile : Dr. Lamwai Masumbuko - Senior Lecturer

MWANASIASA na mwanasheria mkongwe, Dkt. Masumbuko Lamwai amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Mei 5, 2020.

Dkt. Lamwai aliwahi kuwa mbunge wa Ubungo (NCCR-Mageuzi) kabla ya kuhamia CCM na kIsha kuwa mbunge wa kuteuliwa na Rais Benjamin Mkapa.

‪Kabla ya kifo chake, Dkt. Lamwai alikuwa Mhadhiri Mwandamizi (Senior Lecture) katika Chuo Kikuu cha Tumaini akifundisha masomo ya Sheria.

Dkt. Lamwai atakumbukwa kama Mwanasiasa machachari, mwanasheria nguli na mkufunzi mwandamizi (senior lecturer) wa Tumaini University.

Akiwa NCCR-Mageuzi, alikuwa na wanasiasa wengine wakongwe kama Mabere Marando, Marehemu Dk Sengondo Mvungi(RIP), Augustine Mrema, Makongoro Nyerere, Prince Bagenda, Ndimara Tegambwage, Stephen Wassira na wengine wengi.

Katika uchaguzi mkuu wa vyama vingi wa 1995, NCCR-Mageuzi walitetemesha na kutingisha nchi mpaka Mwl. Nyerere akaingilia kati baada kusimama majukwaani CCM.

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani. 
GPL

No comments: