ANGALIA LIVE NEWS
Tuesday, June 30, 2020
Mwanamke Uganda alijifungua baada ya miaka 47 ya ndoa
KAMPALA, UGANDA
Safinah Namukwaya hakutegemea kuwa angekaa miaka 47 bila kupata mtoto baada ya kuolewa
Wakati Safinah alipoolewa na Badru Walusimbi, mkazi wa kijiji cha Nunda huko Lwabenge, katika kitongoji cha Kalungu mwaka 1996, nia yake kuu ilikuwa ni walau kujifungua mtoto mmoja.
Licha ya kuolewa kwa miaka 24, Namukwaya alikuwa hajabarikiwa kupata watoto.
Jitihada za kupata mtoto lilianza kuanzia kwa mwanaume wa kwanza aliyemuoa mwaka 1973 na kuishi naye mpaka 1987, alikuwa anasumbuliwa na tatizo la uzazi kwa mayai kushindwa kukua ndani ya mfuko wa uzazi.
Baada ya kutimiza miaka 45, ndoto zake Namukwaya za kuwa mama zilikufa kabisa.
Machi 2019, wakati anatimiza miaka 63, alitembelewa na wataalamu wa afya ya uzazi ‘ Women’s Hospital International and Fertility Centre’ huko Bukoto, Kampala na kufanyiwa uchunguzi na Dk. Edward Tamale Ssali, ambaye alimweleza kuwa anaweza kujifungua licha ya umri wake kuwa umesonga.
Miezi kadhaa baadae, alipata ujauzito na siku ya Alhamisi (Juni 25, 2020), alijifungua mtoto katika hospitali ya mkoa ya Masaka.
Dakitari wa Hospitali Kuu ya Wilaya ya Masaka Dk. Herbart Kalema alifahamisha gazeti la udaku la Red Pepper kwamba mama huyo alipata matatizo wakati wa ujana wake alipopata mimba lakini walimufanyia upasuaji ambao ulifanyika kimakosa na kusababisha kushindwa kuzaa tena.
Hata hivyo Dk Kalema aliongeza kwamba mama huyo alifanyiwa upasuaji baada ya kukuta mtoto amezungukwa na maji mengi kabla ya kufikisha miezi tisa za kujifungua, mtoto akiwa na miezi minane.
Kulingana na Dk Kalema hali ya mtoto ni nzuri pamoja na mama yake ila mtoto watamutunza kwa majuma matatau kabla ya kuruhisiwa.
Si mwanamke wa kwanza Uganda kujifungua baada ya miaka 50
Alisema gharama yote inagharimu Sh milioni 15 za Uganda lakini Namukwaya alishindwa kupata fedha hizo hivyo alitakiwa kulipa Shmilioni 4 za Uganda.
“Hospitali iliweza kuongezea kiasi cha fedha kilichosalia ili kumfanya mama huyo apate mtoto,”mkurugenzi wa hospitali aliongeza.
Daljinder Kaur pia alijifungua mtoto wake baada ya kupokea matibabu kwa miaka miwili katika hospitali iliyoko jimbo la Haryana nchini India akiwa na umri wa miaka 72.
Daljinder Kaur pia alijifungua mtoto wake baada ya kupokea matibabu kwa miaka miwili katika hospitali iliyoko jimbo la Haryana nchini India akiwa na umri wa miaka 72
Dk Ssali alisema mwanamke yeyote anayekaribia kufika miaka 70 ana uwezo mkubwa wa kuweza kuzaa bado, kwa kusaidiwa kupata mbegu za mume wake na wakati mwingine anaweza hata kupata mayai kutoka kwa mwanamke mwingine.
Namukwaya anakuwa mwanamke wa 25 nchini Uganda ambaye amezidi miaka 50 kupata mtoto kupitia mfumo wa IVF, kwa mujibu wa Dkt Ssali.
Dk Herbert Kalema, mtaalamu wa masuala ya uzazi katika hospitali ya Masaka alisema wakati ambao Namukwaya aliporipotiwa kufika hospitalini hapo wiki tatu zilizopita alikuwa na maumivu, mapigo ya moyo yanaenda kasi alikuwa anapata wakati mgumu kupumua na kutoka jasho kwenye miguu.
“Tulikuwa tunafahamu vizuri historia yake wakati mama huyo alipowasili hospitalini akiwa na miezi nane,hatukutaka ajifungue kawaida ndio maana tulitaka kumfanyia operesheni. Tunamshukuru Mungu kila kitu kilienda sawa,” alisema.
Alisema baada ya operesheni, Namukwaya akawa mwenye nguvu na kuanza kumnyonyesha mtoto wake.
Mtoto alizaliwa akiwa na uzito wa kawaida wa kilo 2.6, alisema Dk Kalema.
“Huyu ni mwanamke wa hamsini ambaye ana umri zaidi ya miaka hamsini kujifungua kwa operesheni na kila kitu kwenda salama,” alisema.
Dk Kalema alisema Namukwaya alihudhuria kliniki katika kituo cha Women’s Hospital International and Fertility Centre, lakini wakati wa marufuku ya kutoka nje kuzuia maambukizi ya corona ilimbidi ahamie hospitali ya Masaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment