ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 29, 2020

SALIM ASAS AWASHIKA MKONO MAJERUHI WA AJALI YA KITONGA.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Salim Abri Asas akiwa na kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi Fortunatus Muslim wakiwajulia hali majeruhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoani Iringa.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

MWENYEKITI wa Kamati ya Usalama Barabarani Salim Abri Asas amewashika mkono majeruhi wa ajali iliyotokea katika mlima Kitonga wilayani Kilolo mkoani Iringa na aliwaombea uponyaji wa haraka majeruhi wanaoendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Ruafa mkoani hapa.

Asas ameliomba Jeshi la Polisi kumtafuta na kumkamata dereva huyo aliyekimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo iliyosababisha vifo na majeruhi kwa watanzania ambao walikuwa wamepanda basi hilo.

Alisema kitendo cha dereva huyo kutokomea kusikojulikana inaaminisha kuwa ajali hiyo ilikuwa ni ya makusudi kwakuwa angekuwepo angetoa ushirikiano mzuri kwa mamlaka zinazohusika

“Huyu dereva ni muuaji haiwezekani iwe ajali ya bahati mbaya harafu akimbie badala ya kutoa ushirikiano kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ningeomba wenzetu wa polisi wamtafute wamkamate na afikishwe katika vyombo vya sheria” amesema Salim Asas

Kwa upande wake kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi Fortunatus Muslim ametembelea majeruhi wanaoendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa baada ya kujeruhiwa katika ajali ya basi la abiria Kampuni ya Prezdar iliyotekea milima ya Kitonga mkoani Iringa

Kamanda Muslim alisema basi hilo lenye naomba za usajili T326 CSX Kampuni ya Prezdar linalofanya safari zake Iringa – Dar es salaam liliatumbukia katika maporomoko ya Milima ya Kitonga wilayani Kilolo.

Kamanda Muslim aliwataka madereva kutambua kuwa wamebeba roho za watu hivyo wanatakiwa kuchukua tahadhari muda wote wanapokuwa barabarani.

Alisema Jeshi la Polisi litaendelea kusimamia sheria za usalama barabarani kwa kuwachukulia hatua madereva wote wanaoendelea kuvunja sharia za usalama barabarani.

Kamanda Muslim alisema jeshi hilo pia linaendelea kumtafuta na kumfikisha katika vyombo vya sheria dereva wa basi hilo ambaye alitokomea kusikojulikana mara tu ilipotokea ajali.

Watu 10 wamepoteza maisha na wengine 36 wamejeruhiwa katika ajali hiyo huku miili 5 ikiwa tayari imetambuliwa na ndugu zao

No comments: