Mifugo mingine iliyokufa baada ya kunywa maji hayo ni punda, bata na paka. Tukio hilo limeripotiwa kutokea juzi katika kijiji cha Mkusa kilichopo katika Kata ya Kilangawana katika Bonde la Ziwa Rukwa katika wilaya ya Sumbawanga na kusababisha taharuki na huzuni kwa waombolezaji waliokusanyika katika nyumba ya mfugaji Elias Juma.
Taarifa kutoka eneo hilo la tukio zinaeleza kuwa katika nyumba ya Juma iliyokuwa na msiba kuna kisima cha maji ambacho alikichimba kwa matumizi ya nyumbani kwa kupikia, kunywa na kunywesha mifugo yake.
Taarifa zilisema kuwa kabla ya waombolezaji hao hawajaanza kuyatumia maji hayo kwa kunywa na kupikia, wanyama hao walichotewa na walipoyanywa walikufa papo hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masejo amethibitisha kuwa tukio hilo lilitokea juzi wakati wakazi wa Kijiji cha Mkusi walipokusanyika msibani kwa mfugaji Juma.
Alisema kuwa watu wawili wamekamatwa na wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa kumwaga sumu katika kisima kilicho jirani na nyumba ya Juma.
Aliongeza kusema kuwa wawili hao ni majirani wa Juma ambapo walishashtakiana mahakamani katika shauri la mgogoro wa ardhi.
“Maofisa Polisi na mtaalamu wa afya walifika kijijini hapo na kufanya uchunguzi wa kitaalamu na kubaini kuwa mifugo hiyo ilikunywa maji yenye sumu ambayo haikuweza kufahamika mara moja,”alieleza. Alithibitisha kuwa hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kupoteza maisha kutokana na tukio hilo.
Akielezea tukio hilo, Juma alisema mifugo yake hiyo wakiwemo ng’ombe wa kisasa 16, punda, bata na paka walikufa papo hapo baada kuyanywa maji hayo.
“Nimepata hasara kubwa kwani ng’ombe wangu 16 wamekufa baada ya kunywa maji hayo, kati yao ni madume matatu ya kisasa aina ya Boran ambao kwa pamoja wana thamani ya Sh 24,900,000 kwani kila mmoja wao ana thamani ya Sh 8,300,000.
Chanzo: HabariLeo
No comments:
Post a Comment