KATIBU wa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, leo Agosti 20, anatangaza majina ya wagombea ubunge wa CCM waliopitishwa na Kamati ya Halmashauri kuu ya Taifa ya chama hicho.
“Vikao vyote cha jana na leo vilikuwa chini ya mwenyekiti wa CCM. Kikao cha halmashauri kuu kilikuwa na lengo moja na limekamilika. Lengo lilikuwa kufanya uteuzi wa mwisho kwa wagombea wa majimbo na viti maalum. Napenda kuleta taarifa hiyo kwenu kwa maana hawa walioteuliwa leo kwa majimbo na viti maalum.
“Walijitokeza 10,367 nafasi za majimbo 264, chama chetu kimeandika rekodi na historia ya kukubalika. Upande wa uwakilishi leo haukufanyika uteuzi kwa sababu ya muingiliano wa ratiba ya NEC. Wagombea 33,094 waliomba kukiwakilisha chama cha mapinduzi kwenye udiwani ilhali nafasi zipo kama elfu nne na kitu na kufanya jumla ya watu 43,461 waliiomba kukiwakilisha chama cha mapinduzi kwenye nafasi mbalimbali.
“Wajumbe wa halmashauri kuu wametimiza wajibu wao na kikao kimeeleza wajibu wao wa kusimamia serikali mpaka tumefika hapa, uamuzi walioufanya leo umezingatia watu wabobevu kusimamia maslahi ya watu wetu watakaofanya kazi sambamba na serikali ya chama cha Mapinduzi ambayo tunaenda kuiombea kura.
“Kwa kauli moja wajumbe wamefanya uteuzi baada ya kupokea majina kwa watakaokuwa wagombea wa CCM kwa nafasi ya ubunge. Vilikuwepo vingezo na sifa ambazo tumezitumia ikiwemo wanaCCM wanaojitoa kwa chama, tumetafuta yule ambae atatuleta pamoja, wenye mahusiano mazuri na wananchi na wanakubalika na jamii.
“Watu ambao wameteuliwa leo wanatakiwa wanatakiwa wafanye maandalizi ya msingi. Kwenye majimbo wanaCCM ni nidhamu tuendelee kuwa watulivu, wagombea ni wengi hatuwezi kupata wote lakini nawahakikishia kwamba, chama chetu ni kikubwa na fursa zake ni nyingi tuendelee kuwa wanyenyekevu na watulivu, chama kina taarifa zenu.
MAJINA WALIOTEULIWA
1. ARUSHA
Arusha Mijini- Mrisho Mashaka Gambo
Arumeru Magharibi- Noah Lebrus Molel
Arumeru Mashariki- John Palangyo
Karatu- Daniel Tlemai
Longido- Stephen Kirusya
Monduli- Fred Lowassa
Ngorongoro- Ole Nasha
2. DAR
Ubungo- Prof Kitila Kitila
Kibamba- Issa Jumanne Mtemvu
Kinondoni- Abass Tarimba
Kawe- Askofu Josephat Gwajima
Kigamboni- Dr. Faustine Ndugulile
Ilala- Mussa Zungu
Segerea- Bonna Kamoli
Ukonga- Jerry Slaa
Temeke- Doroth Kilave
Mbagala- Abdallah Chaurembo
3. DODOMA
Bahi- Keneth Nolo
Chamwino- Deo Dejembi
Mvumi- Livingstone Lusinde
Chemba- Mohammed Moni
Dodoma Mjini- Anthony Mavunde
Kongwa- Job Ndugai
Kondoa mji- Ally Juma Makoa
Kondoa Vijijini- Dr. Ashatu Kijaji
Kibakwe- George Simbachawene
Mpwapwa- George Nataly Malima
4. GEITA
Busanda- Tumaini Magesa
Geita Mjini- Consatantine Kanyasu
Geita vijijini- Joseph Kasheku(Musukuma)
Bukombe- Dotto Bisheko
Chato- Medard Kalemani
Mbogwe- Nicodemas Maganga
Nyang’alwe- Hussein Amar
5. IRINGA
Iringa Mjini- Jesca Msavatambangu
Kalenga- Jackson Kiswaga
Isimani- William Lukuvi
Kilolo- Lazaro Nyamoga
Mafinga mji- Cosato Chumi
Mufindi Kaskazini- Exaud Kigahe
Mufindi Kusini- David Kihenzile
6. KAGERA
Bukoba mjini- Stephen Byabato
Bukoba vijijini- Jackson Rweikiza
Nkenge- Frolent Kyombo
Karagwe- Innocent Bashungwa
Kyerwa- Innocent Bilakwate
Ngara- Ndaisaba Luhoro
Bihalamuro- Ezra Chiwelesa
Muleba Kaskazini- Charls Mwijage
Muleba Kusini- Oscar Kikoyo
7. KATAVI
Mlele- Isack Kamwele
Kavuu- Geophrei Mizengo Pinda
Mpanda Mjini- Sebastian Kapufi
Nsimbo- Anna Lupembe
Mpanda Vijijini- Moshi Kakoso
8. KIGOMA
Kasuli Mjini- Prof Joyce Ndalichako
Manyovu- Dr. Philip Mpango
Buyungu- Aloyce Kamamba
Muhambwe- Atashasta Nditiye
Kigoma Mjini- Kirumbe Shabani Ng’enda
Kigoma Kaskazini- Asa Nelson Makanika
Kigoma Kusini- Nashon William
Kasulu vijijini- Augustine Hole
9. KILIMANJARO
Vunjo- Charls Kimei
Siha- Dr. Godwin Mollel
Moshi Vijijini- Prof. Patrick Ndakidemi
Hai- Salasisha Mafue
Same Mashariki- Anne Kilango Malecela
Same Magharibi- Dr. Mathayo David Mathayo
Rombo- Prof. Adolf Mkenda
Moshi Mjini- Priscus Tarimo
Mwanga- Anania Tadayo
10. LINDI
Kilwa Kaskazini- Ndulane Franscis
Kilwa Kusini- Kasinge Mohammed Ally
Liwale- Zuberi Kuchauka
Lindi Mjini- Hamida Mohammed Abdallah
Mchinga- Salma Kikwete
Mtama- Nape Nnauye
Nachingwea- Amandus Julius Chinguiye
Ruangwa- Kassim Majaliwa
11. MANYARA
Babati Mijini- Paulina Gekul
Babati vijijini- Daniel Silo
Hanang- Samwel Kadai
Mbulu mji- Isai Paulo
Mbulu vijijini- Flatei Gregory
Kiteto- Edward Kisau
Simanjiro- Christpher Ole Sendeka
12. MARA
Musoma Mjini- Vedastus Manyinyi
Musoma Vijijini- Prof. Sospeter Muhongo
Bunda Mjini- Robert Chacha Maboto
Bunda Vijijini- Boniface Getere
Mwibara- Charls Kajege
Butiama- Jumanne Sagini
Rorya- Jaffary Wambura Chege
Tarime Mjini- Mwita Michael Kembaki
Tarime Vijijini- Mwita Waitara
Serengeti- Dr. Jeresabi Mkimi
13. MBEYA
Busekelo- Atupele Mwakibete
Kyela- Ally Jumbe
Lupa- Masache Kasaka
Mbalali- Franscis Mtega
Mbeya Mjini- Dk. Tulia Akson
Mbeya Vijijini- Oran Njeza
Rungwe- Anthony Mwantona
14. MOROGORO
Mlimba- Godwin Kunambi
Kilombero- Abubakar Asenga
Morogoro mjini- AbdulAziz Abood
Gairo- Ahmed Shabiby
Malinyi- Antipas Mgungusi
Morogoro Kusini- Innocent Kalogeres
Morogoro Mashariki- Hamis Shaaban Taletale
Mvomero- Jonas Vanzilad
Mikumi- Deniss Lazaro Londo
Kilosa- Prof. Palamaganda Kabudi
Ulanga- Salim Hasham
15. MTWARA
Mtwara Mjini- Mtenga Hassan Selemani
Mtwara Vijijini- Hawa Ghasia
Nanyamba- Abdallah Chikota
Tandahimba- Katani Katani
Newala mjini- George Mkuchika
Newala Vijijini- Maimuna Mtanda
Masasi- Geofrey Mwambe
Lulindi- Issa Mchungahela
Ndanda- Cecil David Mwambe
Nanyumbu- Yahaya Ali Mhata
16. MWANZA
Ukerewe- Joseph Mkundi
Ilemela- Dkt. Angelina Mabula
Sengerema- Tabasamu Hamis Mwagao
Buchosa- Erick Shigongo James
Nyamagana- Stanslaus Mabula
Misungwi- Alexander Mnyeti
Sumve- Kasalali Emmanuel Mageni
Kwimba- Shanif Mansour
Magu- Bonaventura Kiswaga
17. NJOMBE
Lupembe- Edwin Sware
Makambako- Deo Sanga
Njombe Mjini- Deodatus Mwanyika
Makete- Festo Sanga
Wanging’ombe- Dk. Festo John Dugange
Ludewa- Kamonga Zakarius
18. PWANI
Bagamoyo- Muharami Mkenge
Chalinze- Ridhwan Kikwete
Kibiti- Twaha Mpembenue
Kibaha Mjini- Sylvester Koka
Kisarawe- Selemani Jaffo
Mkuranga- Abdallah Ulega
Mafia- Omar Kipanga
Rufiji- Mohammed Mchengelwa
Kibaha Vijijini- Michael Mwakamo
19. RUKWA
Nkasi Kusini- Vicent Mbogo
Sumbawanga Mjini- Ayeshi Hilal
Kwera- Deus Sangu
Nkasi Kaskazini- Ally Kessy Alimabodi
Kalambo- Josephat Kandege
20. RUVUMA
Songea Mjini- Dkt. Damas Ndumbaro
Peraminho- Jennister Mhagama
Madaba- Joseph Mhagama
Nyasa- Stella Manyanya
Mbinga Mjini- Jonas Mbunda
Mbinga Vijijini- Benaya Kapinga
Namtumbo- Vita Kawawa
Tunduru Kaskazini- Hassan Kungu
Tunduru Kusini- Daim Mpakate
21. SHINYANGA
Shinyanga mjini- Patrobas Katambi Paskal
Solwa- Ahmed Salum
Kahama Mji- Jumanne Kishimba
Msalala- Idd Kassim Idd
Ushetu- Elias Kwandikwa
Kishapu- Boniface Butondo
22. SIMIYU
Bariadi- Andrea Mathew
Busega- Saimon Songe
Itilima- Njalu Daud Silanga
Maswa Magharibi- Mashimba Ndaki
Maswa Mashariki- Nyongo Stanslaus Harun
Meatu- Leah Komanya
Kisesa- Luhaga Mpina
23. SINGIDA
Singida Mjini- Mussa Sima
Singida Kaskazini- Ramadhan Ihondo
Singida Mashariki- Miraji Jumanne Mtaturu
Singida Magharibi- Elbariki Kingu
Manyoni Mashariki- Dkt Stephen Chaya
Manyoni Magharibi- Yahaya Omar Masare
Iramba Mashariki- Franscis Isack Minga
Iramba Magharibi- Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba
24. SONGWE
Ileje- Geofrey Kasekenya
Mbozi- George Mwenisongole
Vuawa- Japhet Hasunga
Tunduma- David Ernest Silinde
Momba- Kondesta Sichalwe
Songwe- Philipo A. Mulugo
25. TABORA
Igunga- Nocholaus Ngassa
Manonga- Seif Hamis
Tabora Kaskazini- Athumani Mahige
Igalula- Venant Protas
Tabora Mjini- Emmanuel Mwakasaka
Nzega Mjini- Hussein Bashe
Nzega Vijijini- Hamis Kigwangallah
Bukene- Selemani Jumanne
Kaliua- Aloyce Kwezi
Uliankulu- Rehema Migila
Urambo- Magreth Sitta
Sikonge- Joseph Kakunda
26. TANGA
Bumbuli- January Makamba
Korogwe Mjini- Alfred Kimea
Korogwe Vijijini- Timotheo Paul Mnzava
Pangani- Jumaa Aweso
Lushoto- Shaban Shekilindi
Handeni Mjini- Kwagila Mhamanilo
Handeni Vijijini- John Salu
Kilindi- Omar Kigua
Tanga Mjini- Ummy Mwalimu
Mlalo- Rashid Shangazi
Muheza- Hamis Mwinjuma(MwanaFA)
Mkinga- Dastan Kitandula
No comments:
Post a Comment