Saturday, November 7, 2020

WAREMBO 20 KUANZA KAMBI YA MISS TANZANIA TAREHE 26 NOVEMBA 2020.


Warembo 20 kutoka Kanda 5 za mikoa ya Tanzania wanatarajia kuanza kambi ya mchuano wa Fainali za Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania tarehe 26 Novemba 2020 jijini D’salaam.

Hatua za awali za mashindano haya ulianza mapema mwezi Februari mwaka huu, baadae mchakato ulisitishwa kidogo kutokana na janga la ugonjwa wa Corona ulioikumba nchi yetu pamoja na dunia kwa ujumla.

Mchakato wa kuwapata washiriki 100 wa awali uliendelea mwezi Juni mara baada ya tishio la ugonjwa wa virus vya Corona kumalizika, ambapo mchujo wa washiriki 100 ulifanyika na kuwapunguza hadi washiriki 50.

Washiriki 50 walipewa majukumu ya kufanya na kuwasilisha majibu yake kwa Wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania ambao ndio walikuwa na jukumu la kudadisi na kuperuzi majibu ya washiriki wote.

Kati ya washiriki 50 ni washiriki 20 tu ndio waliopita katika mchakato huo, nao wameshajulishwa tayari kuhusu kuingia kambi ya Miss Tanzania mwisho wa mwezi Novemba.

Majina ya washiriki hao pamoja na umri wao ni kama ifuatavyo:-
PRISCA LYIMO umri miaka 22
TAMIA HAKAM miaka 19
JULIANA RUGUMISA miaka 23
REHEMA CUTHBERT miaka 21
YVONNE PAUL miaka 20
RUTH BENITHO miaka 23
GRACE MACHIBULA miaka 24
ROSE MANFERE miaka 20
MARGARET MWAMBI miaka 23
SARAFINA MAGEYE miaka 20
MARTHA GOLODI miaka 23
ZENITHA CHUNDU miaka 22
DEOLYN MOLLEL miaka 21
HOYCE BAKANOBA miaka 20
NECERIAN KIVUYO miaka 20
RAZIA ABRAHAM miaka 19
ANGELA PENDAELI miaka 23
ADVERA MWEMBA miaka 21
VERYNICE DEOKARI miaka 24
GLORIA FELA miaka 23

Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania yanaandaliwa na Kampuni ya The Look chini ya Mkurugenzi wake Bi. Basilla Mwanukuzi Shayo. Miss Tanzania 1998.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake