POLISI Mkoa wa Dar es Salaam imemkamata Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula wa Kanisa la Uamsho la Moravian kwa kosa la kuhamasisha maandamano nchi nzima kupitia mitandao ya kijamii.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema taarifa ya Mwamakula iliyokuwa ikihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuandamana kushinikiza na kudai #Katiba mpya ni kinyume na taratibu na sheria za nchi na kwamba jambo hilo lingeleta taharuki kwa umma.
No comments:
Post a Comment