Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James akiwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti wakisaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma Katika ni Mwanasheria wa Wizara ya Fedha Bi.Loveness Msechu akishuhudia.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James akiwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti wakionyesha mikataba mara baada ya Serikali kusaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James akipongezana na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti mara baada ya kusaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
Baadhi ya Makatibu wakuu kutoka wizara mbalimbali wakifatilia utiaji saini wa mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti ,akizungumza mara baada ya kusaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 kwa Kuipa Tanzania fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdeo ,akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji wa mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Aloyce Nzuki,akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji wa mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi.Amina Shaaban ,akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James ,akiwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna,Dodoma
SERIKALI imesaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti ikiwa ni sehemu ya mpango wa ushirikiano wa 11 chini ya mfuko wa maendeleo wa Ulaya.
Akizungumza baada ya kusaini mikataba hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James amesema fedha hizo zitaelekezwa kwenye miradi hiyo sita ambayo ni Mradi wa kuboresha Sekta ya Nishati ambayo kiasi cha Sh Bilioni 96.7 kimetengwa kwa ajili yake, Mradi wa Matumizi Endelevu ya Nishati ya Kupikia ambao utagharimu Sh Bilioni 82.8 na mradi wa Kusaidia Mnyororo wa Thamani katika Ufugaji Nyuki ambao umetengewa kiasi cha Sh Bilioni 27.6.
Miradi mingine ni mradi wa Kuboresha Afya ya Miaka Nchini ili kuongeza usalama wa chakula ambao utagharimu kiasi cha Sh Bilioni 27.6, Mradi wa Kusaidia Kuboresha Mazingira ya Biashara, Ukuaji na Ubunifu ambao thamani yake ni Sh Bilioni 63.5 na Mradi wa Ushirikiano wa Kitaalamu ambao kiasi cha fedha kilichotengwa ni Sh Bilioni 9.7 na kufanya jumla ya miradi yote kuwa Sh Bilioni 307.
Bw. James amemshukuru Balozi wa Ulaya nchini, Manfredo Fanti kwa msaada huo ambao hauna masharti yoyote jambo ambalo linaonesha jinsi gani Umoja wa Ulaya na Tanzania wamekua na mahusiano mazuri huku akimhakikishia kuwa fedha hizo zitatumika kama ambavyo makubaliano ya mkataba huo yameelekeza.
” Nikiri wazi kwamba Umoja wa Ulaya ni wadau wetu wakubwa wa kimaendeleo na kupitia misaada hii inayotolewa nao chini ya Mpango wa 11 imeeelekezwa kutatua mahitaji na changamoto zilizoainishwa katika mpango ya maendeleo ya kitaifa hususani mpango wa pili wa maendeleo (FYDP II) 2016/17 – 2020/21 na MKUZA II na misaada iliyotolewa leo imezingatia mahitaji yetu na changamoto zilizoainishwa kwenye mipango ya maendeleo ya kitaifa.
Kwa niaba ya Serikali yetu niwashukuru sana EU kwa misaada yao kwetu kwani imekuja wakati muafaka ambapo Serikali inaweka mazingira wezeshi ya kukuza viwanda kwa ajili ya ukuaji uchumi wetu, ” Amesema James.
Aidha amesema kuwa mpango wa tatu wa maendeleo wa miaka mitano (FYDP III) ambao uko katika maandalizi pamoja na Dira ya Maendeleo 2050 iliyoidhinishwa hivi karibuni kwa upande wa Zanzibar ni nyenzo muhimu katika uandaaji wa mpango ujao wa ushirikiano wa maendeleo baina ya Tanzania na Umoja huo.
Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti ameipongeza serikali ya Tanzania kwa namna ambavyo imekua ikitekeleza miradi yote ambayo inashirikiana na Umoja huo jambo ambalo linazidi kukuza mahusiano yaliyopo baina ya pande hizo mbili.
” Ni wazi kwamba mikataba hii ni viashiria vya namna ambavyo Serikali ya Tanzania na EU tumekua tukishirikiana bila vikwazo, tuna furaha kuona kuwa kama Serikali mmekua mkitekeleza miradi tunayoshirikiana kwa kufuata mikataba yetu, ahadi yetu ni kwamba mashirikiano yetu na nyie yataendelea kuwepo,” Amesema Bw.Fanti.
No comments:
Post a Comment