ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 5, 2021

WAKUU WA MIKOA WAMLILIA AYEKUWA KATIBU TAWALA MKOA WA ARUSHA, WASISITIZA MADEREVA KUFUATA SHERIA ZA BARABARANI

Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddi Kimanta akitoa heshima za mwisho ya kuaga mwili wa aliyekuwa katibu tawala wa mkoa wa Arusha marehemu Richard Kwitega.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mgwira akitoa heshima za mwisho ya kuaga mwili wa aliyekuwa katibu tawala wa mkoa wa Arusha marehemu Richard Kwitega.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Loota Ole Sanare akitia heshima mwisho ya kuaga mwili wa aliyekuwa katibu tawala wa mkoa wa Arusha marehemu Richard Kwitega.

NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Anna Mgwira amewataka madereva kufuata sheria na kanuni za barabarani ,Ili kulinda usalama wao wenyewe , abiria pamoja na wanaotumia barabara .

Aliyasema hayo leo Katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid wakati wa zoezi la kuuaga mwili wa aliyekuwa katibu tawala mkoa wa Arusha Richard Kwitega aliyefariki dunia February 3 mwaka huu kutokana na ajali ya gari ulipotokea katika eneo la Mdori lililopo wilaya Babati mkoani Manyara.

Alisema kuwa asilimia kubwa ya ajali hii iliyoondoa maisha ya Kwitega imesababishwa ukiukwaji wa sheria za barabarani za madereva hivyo nivyema madereva wakajitaidi kuchukuwa taathari na wajitaidi kulinda usalama wao,usalama wa abiria waliowabeba na hata wale watembea kwa miguu wanaotumia barabara.

“Nipende kuwaambia familia muombeni Mungu na naomba tumuombe Mungu amnyanyue mtu atakae ridhi mikoba yake ,atakayeweza kufuata nyayo zake na atakaye ziba pengo lake”alisema Mgwira.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddi Kiman’ta alisema kuwa msiba huu ni mkubwa mno kwa wana Arusha kwani wote wanafahamu ni namna gani mkoa umekuwa ukifanya vizuri katika sekta mbalimbali ambapo alibainisha chanzo cha kufanya vyema ni Kwitega ambaye ndio alikuwa Msimamizi mkuu wa utendaji wa shughuli za serikali.

“Nasema haya si kumfurahisha mtu bali nasema uhalisia wake alikuwa ni mtu ambaye ni mtulizaji wa mambo ,hata kuwepo na jambo gumu kiasi gani kikifika ofisini kwake litapata ufumbuzi ,alikuwa ni mtu mwenye kujenga hoja,alikuwa na upendo na mwenye kuheshimu mamlaka hivyo nipende kusisitiza tuache chuki ,tuache fitina na majungu na tupendane , Richard nenda , Richard nenda ndugu yangu wengine tupo tunakuja tupo nyuma yako ,nenda kakake upande wa kulia wa baba na sisi tunakuja katuandalie makao twaja”alisema Kiman’ta.

Kwa upande mkuu wa mkoa wa Morogoro Loota OkeSanare alisema kuwa Kwitega alikuwa ni zaidi ya kiongozi hapa Arusha hasa wakati ambapo siasa zilikuwa moto haikubali jambo lolote liharibike au lisiwekwe sawa ,alieleza namna ambavyo serikali inatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ,lakini pia alifanya kazi Arusha huku akitumika Katika mikoa mingine.

Naye msemaji wa familia ya Kwitega ,Christooher Nkisi aliushukuru uongozi wa mkoa wa Arusha pamoja na Manyara na serikali kwa ujumla kwajinsi walivyoweza kumsitiri na kumuhifadhi ndugu yao tangu pale alipopata ajali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha (APC)Claud Gwandu alisema kuwa kwa kutambua mchango mkubwa wa marehemu katibu tawala ,katika sherehe za kuazimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari wanaanzisha tuzo za kiongozi bora , hivyo kwa heshima na kutambua mchango wake tuzo ya mwaka huu watampa yeye ambaye alikuwa ni mwanga katika utendaji wa viongozi mkoa wa Arusha .

marehemu Richard Kwitega alozaliwa agast 15 ,1965 Katika Kijiji Cha Ngoma wilayani Sengerema mkoani Mwanza ameacha mjane na watoto wanne ,wawili wa kiume na wawili wa kike.

No comments: