Advertisements

Tuesday, March 9, 2021

Mhe.Ulega: Usikivu wa TBC Unaendelea Kuimarika

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Abdallah Ulega akizungumza leo Machi 9, 2021 Bungeni Jijini Dodoma na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa kupokea taarifa kuhusu Mradi wa ujenzi wa studio ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mikocheni Dar es Salaam na Ujenzi wa redio ya jamii Makao makuu Jijini Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ally Possi akizungumza jambo Bungeni Jijini Dodoma na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa kupokea taarifa kuhusu Mradi wa ujenzi wa studio ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mikocheni Dar es Salaam na Ujenzi wa redio ya jamii Makao makuu Jijini Dodoma leo Machi 9, 2021
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayoub Ryoba akiwasilisha taarifa kuhusu Mradi wa ujenzi wa studio ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mikocheni Dar es Salaam na Ujenzi wa redio ya jamii Makao makuu Jijini Dodoma kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Bungeni Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe.Stanslaus Nyongo akiongoza kikao cha Kamati hiyo na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakati wa wa kupokea taarifa kuhusu Mradi wa ujenzi wa studio ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mikocheni Dar es Salaam na Ujenzi wa redio ya jamii Makao Makuu Jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Abdallah Ulega akizungumza jambo na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayoub Ryoba mara baada ya kikao kati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa kupokea taarifa kuhusu Mradi wa ujenzi wa studio ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mikocheni Dar es Salaam na Ujenzi wa redio ya jamii Makao makuu Jijini Dodoma,Wa pili Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ally Possi

Picha na MAELEZO

Na Shamimu Nyaki – WHUSM

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Abdallah Ulega amesema kwamba Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) linaendelea kuimarisha usikivu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa studio za Televisheni ya TBC, Mikocheni Dar es Salaam.

Mhe. Ulega ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya jamii ilipopokea taarifa kuhusu mradi wa ujenzi wa studio hiyo pamoja na ujenzi wa Redio ya Jamii Makao Makuu Jijini Dodoma.

“Taarifa inayowasilishwa kwenu leo itawezesha kupatikana uelewa wa hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi hii na mtakapoitembelea mtapata fursa ya kuona hali halisi ya utekelezaji” alisema Mhe.Ulega.

Akiwasilisha taarifa hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Ryoba ameeleza kuwa katika bajeti ya miradi ya maendeleo ya takriban Shilingi milioni 900 iliyoidhinishwa, pamoja na shilingi bilioni 1 kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) zilitekeleza uboreshaji wa mfumo wa umeme na ufungaji wa “AVR na UPS,” ununuzi na ufungaji wa mitambo na vifaa vya redio pamoja na ukarabati wa jengo la studio.

“Baada ya uboreshaji kupitia fedha hizo manufaa mbalimbali yamepatikana ikiwemo kuaandaa na kurusha vipindi vya redio na televisheni kutokea Dodoma, matangazo ya televisheni ya kipindi cha ARIDHIO na Jambo Tanzania yamekuwa yakirushwa kutokea Dodoma” Alisema Dkt.Ryoba.

Dkt. Ryoba aliongeza kuwa, manufaa mengine yaliyotokana na mradi huo ni kurushwa mbashara vipindi vinavyohitaji ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kitaifa kutoka kwa viongozi wa Serikali muda wote inapohitajika kufanya hivyo pamoja na redio jamii kuhusika kurusha habari za kikanda hivyo kuleta uelewa kwa wananchi kuhusiana na kazi wanazofanya.

MWISHO…


No comments: