Advertisements

Saturday, April 17, 2021

DENNIS MAKUNDI MGOMBEA UHAZINI JUMUIA YA WATANZANIA DMV

Hazina ni usimamizi wa Fedha katika jumuiya, na kipaumbele changu nitahakikisha kwamba nitasimamia pesa yote ya jumuiya na itatumika kufanya tu kile ambacho jumuiya imekusudia kufanya.
Kwa kufanya hivyo naamini nitakuwa naendeleza mikakati na sera za kifedha kwa muda mrefu ambapo zitaleta matukio chanya katika jumuiya yetu. Uweka hazina wangu utakuwa ni kushuhulikia takwimu na pesa, pia ujuzi mzuri katika mawasiliano na mengineyo.

Nitahakikisha maamuzi yote ya kifedha yanachukuliwa na kufuatiliwa kulingana na katiba yetu ya jumuiya isemavyo.

Hazina inahitaji kuwa na maamuzi mazuri ya usimamizi mzuri wa fedha pamoja na miundo yake hii ni pamoja mkusanyiko mzuri wa pesa ujumlishaji wa namba na uhifadhi ulio bora na salama.

1. Mimi mwenyewe binafsi ninauwezo mkubwa wa kushuhulikia takwimu pamoja na fedha taslimu.
2. Nina akili pamoja na njia nzuri na bora ya kufikiria ya kimfumo wa kisasa ambao unaendana na Dunia ya leo.
3. Ninauwezo katika kushuhulikia pesa nyingi na bajeti.
4. Nina uzoefu wa udhibiti wa kifedha na bajeti.
5. Niko tayari kupokea ushauri wa kifedha na takwimu kutoka kwa mwanachama yeyote hai wa jumuiya yetu kwa manufaa ya jumuiya yetu.

Niko tayari kusimamia Hazina yetu kwa nguvu zangu zote na kwa akili zangu zote na naahidi kutii na kufuata katiba yetu ya jumuiya yetu ya D.M.V. Asanteni.

Vote#Treasury#Dennis



 

No comments: