Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akipata maelezo mafupi kutoka kwa Afisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Gabriel Girangay (katikati), kuhusu ushiriki wa BRELA katika maonesho ya SIDO Kanda ya Kaskazini, yanayofanyika katika viwanja vya Kwaraa, vilivyopo mjini Babati Mkoani Manyara. Maonesho hayo yameanza Mei 27 hadi Mei 31 mwaka 2021.Karibu tukuhudumie.
Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye akisaini katika kitabu cha wageni katika banda la BRELA katika maonesho ya SIDO yanayofanyika katika viwanja vya Kwaraa, vilivyopo Mjini Babati, maonesho hayo yameanza Mei 27 na yatamalizika Mei 31 mwaka 2021. Karibuni tuwahudumie.
Na Christina Njovu, Manyara
NAIBU
Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amewataka wananchi
na wajasiriamali katika Mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga
kutembelea katika mabanda ya washiriki wa maonesho ya SIDO kanda ya
Kaskazini yanayofanyika katika viwanja vya Kwaraa mjini Babati.
Lengo
likiwa ni kupata huduma zinazotolewa na washiriki wa maonesho hayo
ikiwemo Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni( BRELA).
Kigahe
amesema hayo alipokuwa akifungua maonesho ya SIDO Kanda yaKaskazini
yanayofanyika katika viwanja hivyo baada ya kutembelea mabanda ya
washiriki wa maonesho hayo na kuzungumza na baadhi ya wajasiriamali
ambao wamemuomba kusaidia kutatua changamoto wanazokabiliana nazo.
Pia
wamemuomba kusaidia kuharakisha upatikanaji wa huduma ambazo
wanazihitaji zikiwemo kusajili biashara zao, kupata nembo za ubora na
pia kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na Taasisi za umma.
“Tembeleeni
maonesho haya ili muweze kujifunza na kufahamu umuhimu wa kusajili
Majina ya Biashara na Makampuni pia mtaweza kusajili Majina ya Biashara
na Makampuni yenu hapa hapa uwanjani katika banda la BRELA ambao nao ni
miongoni mwa washiriki katika maonesho haya.
"Pia mtaweza kujua
mbinu za kutafuta masoko ya bidhaa, fursa za masoko zilizo wazi nchini
na mikakati ya kushiriki maonesho mbalimbali yanayoandaliwa na SIDO na
mashirika mengine,” amesema Kigahe.
Aidha ameongeza wajasiriamali
wakiweza kupata mafunzo hayo hivi sasa yatawawezesha kupata ushiriki wa
kimkakati kwakuwa yatawawezesha kushiriki katika maonesho mbalimbali ya
kitaifa na kimataifa kwakuwa suala la kufanya biashara ni endelevu
Na
kwamba linahitaji elimu kila wakati na kuwasihi wafunguke na waendelee
kutafuta elimu hususani kutoka shirika la viwanda vidogo SIDO ili
Biashara zao zizidi kukua.
Awali Naibu Waziri Kigahe alitembelea
banda la BRELA ambalo ni miongoni mwa mabanda ya washiriki katika
maonesho hayo alipata maelezo juu ya sababu ya ushiriki wa wakala
katika maonesho hayo kutoka kwa Afisa Usajili wa Wakala wa Biashara na
Leseni (BRELA) Gabriel Girangay ambaye amemueleza Naibu Waziri Mh.Exaud
Kigahe kuwa;
“BRELA imeshiriki katika maonesho ya SIDO kanda ya
Kaskazini ili kusogeza huduma zetu karibu, huduma zetu zinatolewa kwa
njia ya mtandao huduma hizo ni pamoja na Usajili wa Makampuni,
Usajili wa Majina ya Biashara, Usajili wa Alama za Biashara na Huduma”.
Girangay
aliongeza kuwa; "Vile vile tunatoa Hataza ambayo ni hati miliki
Ubunifu, Utoaji wa Leseni za Biashara kundi A, Utoaji wa Leseni za
Viwanda”.
Ushiriki huu unatoa fursa kwa Wananchi wa Mkoa wa
mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga wanaohitaji kupata sajili
mbali mbali ama waliokuwa wakipata changamoto za kufanya sajili kwa
njia ya mtandao kuweza kupata huduma moja kwa moja.
Maonesho
haya yaliyoanza jana tarehe 27 Mei yanatarajiwa kufungwa tarehe 31 Mei
,2021 yanawakutanisha wananchi wa mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro
na Tanga.
BRELA inawakaribisha wananchi wote kutembelea banda lake ili waweze kuhudumiwa. 'BRELA tunaipa utu wa kisheria biashara yako'.
No comments:
Post a Comment