Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Mhe. Cristine Musisi (kushoto) ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula akizungumza huku Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) Mhe. Cristine Musisi akimsikiliza ofisini kwake
Mtumba jijini Dodoma Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) Mhe. Cristine Musisi baada ya kumaliza mazungumzo yao
ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (katikati) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Mhe. Cristine Musisi (kushoto) huku
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Mteule Makocha
Tembele akishuhudia mazungumzo hayo yaliyofanyika katika mji wa Serikali
jijini Dodoma.
**************************
Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula
(MB) amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Mhe. Cristine Musisi ofisini kwake
Mtumba jijini Dodoma.
Katika mazungumzo hayo Viongozi hao
wamejadiliana na kukubaliana kuendelea kuimarisha mahusiano kati ya UNDP
, Wizara ya Mambo ya Nje na Serikali ya Tanzania ili kuhakikisha lengo
la kupatikana kwa maendeleo linafikiwa kwa pamoja.
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mulamula
alimuhakikishia Bibi Musisi utayari wa Tanzania katika kuimarisha
mahusiano na UNDP na kumueleza kuwa Serikali ya Tanzania imejipanga
kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa vitendo.
Mhe. Waziri pia
amemuhakikishia Bibi Musisi kuwa Wizara yake inatilia mkazo kauli ya
Serikali ya kuvutia na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kufanya
biashara nchini ili kuvutia wawekezaji na wafanya biashara kuja kuwekeza
nchini kwa maendeleo ya Taifa.
Mhe Waziri alisisitiza kuwa
Wizara inatilia mkazo pia suala la kuwajengea ujuzi wataalamu wake
katika maeneo ya teknolojia ya habari na mawasiliano ili kwenda na
wakati na hivyo kuendesha na kushiriki mikutano kwa njia ya mtandao hasa
wakati huu wa ugonjwa wa CCOVID 19, ujuzi wa kufanya uchambuzi na namna
bora ya kuwasiliana ili kuhakikisha Tanzania inanufaika na utekelezaji
wa diplomasia ya uchumi..
Naye Mwakilishi Mkazi wa UNDP Mhe.
Musisi alimuhakikishia Mhe. Waziri Mulamula kuwa UNDP ipo tayari na
itaendelea kushirikiana na Wizara kwa karibu na Wizara ikiwa ni pamoja
na kutoa wataalam na mafunzo kwa watendaji wa Serikali ili kuendeleza
ujuzi wa watendaji serikalini na kuwafanya kutoa huduma bora zaidi kwa
Taifa na wananchi wake.
Amesema UNDP itandelea kusaidia utoaji wa
mafunzo, kuendesha na kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa
ajili ya maendeleo ya Watanzania na Tanzania ujumla.
No comments:
Post a Comment