ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 22, 2021

RC PWANI AWAPA UJUMBE WAKUU WA WILAYA WAPYA BAADA YA KUAPISHWA

Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Abubakar Kunenge akizungumza baada ya kuwaapisha wakuu wa wilaya ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Khadija Nassir Ali, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,Nickson Saimon na Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Canal Ahmed Abas, Kunenge, kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa huo iliyopo mjini Kibaha.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Khadija Nassir Ali kulia akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Abubakar Kunenge wakati wakiapishwa wakuu wa wilaya za mkoa huo kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa huo iliyopo mjini Kibaha.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Khadija Nassir Ali  akisaini kiapo
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,Nickson Saimon kulia akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Abubakar Kunenge wakati wakiapishwa wakuu wa wilaya za mkoa huo leo kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa huo iliyopo mjini Kibaha.
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Canal Ahmed Abas  kulia akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Abubakar Kunenge wakati wakiapishwa wakuu wa wilaya za mkoa huo leo kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa huo iliyopo mjini Kibaha.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Wakuu wa wilaya wakila kiapo cha utii na utumishi na kuilinda nchi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Abubakar Kunenge hayupo.


Viogozi  wa Mkoa wa Pwani na wageni wakishiriki kuimba wimbo wa Taifa 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani,Mohamed Mwela(kushoto) akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Khadija Nassir Ali baada ya kula kiapo leo  kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa huo iliyopo mjini Kibaha .



 MKUU wa Mkoa  Pwani Abubakar Kunenge amewaapisha wakuu wa wilaya watatu  kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa majukumu yao ya kuwahudumia wananchi huku akiwasisitiza kuhakikisha wanafanya kazi kama timu moja.


Akizungumza baada ya KUwaapisha wakuu wa Wilaya ,ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Khadija Nassir Ali, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,Nickson Saimon na Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Canal Ahmed Abas, Kunenge amesema "Nawaapisha leo ili mkatekeleze majukumu yenu lakini kumbukeni kubwa ni kufanya kazi kwa timu ili muweze kufanikiwa kwa utekelezaji wa mahitaji ya wananchi."
 
 Kunenge amesema siri kubwa ya mafanikio katika utendaji wao  ni kujenga mahusiano mazuri na wanachama wa chama Cha Mapinduzi kwani wao ndio wenye ilani wanayoitekeleza.
 
 Aidha amewataka wakuu wa wilaya wote ndani ya Mkoa huo kuhakikisha wanatatua changamoto za wananchi kabla ya kufika kwake na kama ikifika kwake iwe ni ushauri tu.

"Niwatahadharishe wananchi wenye tabia ya kuvamia mashamba yaliyo wazi na kugawana,mnatakiwa kutambua hakuna eneo lisilo na watu hivyo tabia hiyo ife mara moja katika Mkoa wetu.

" Rais Samia Suluhu Hassan amewaamini naa kuwapa nafasi ya kuwa wasaidizi wake katika ngazi ya wilaya hivyo kila mmoja wenu ajitume kwenye kutatua changamoto za wananchi waliompigia kura,"amesema  Kunenge.

No comments: