Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani Nchini Tanzania (WHO) Dkt. Tigest Ketsela Mengestu akifanyiwa vipimo kwa ajili ya kuchangiaji damu katika siku ya uchangiaji duniani ambayo hufanyika kila Juni 14 ya kila mwaka iliyofanyika ofisi za umoja huo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani Nchini Tanzania (WHO) Dkt. Tigest Ketsela Mengestu akizungumza kuhusiana na umuhiu wa uchangiaji damu katika siku ya uchangiaji duniani ambayo hufanyika kila Juni 14 ya kila mwaka ,iliyofanyika ofisi za umoja huo jijini Dar es Salaam.
Umoja wa Mataifa Tanzania wameshiriki Siku ya Uchangiaji Damu Duniani ambayo hufanyika kila Juni 14 ya kila mwaka ikiwa ni kwa ajili ya kuokoa maisha wahitaji wa damu. Umoja wa Mataifa Tanzania (UN) wameanya zoezi la uchangiaji damu zimefanyika katika ofisi umoja huo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika siku ya uchangiaji damu Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Zlatan Milišić amewashukuru watoaji wa damu wa hiari hiari kwa ajili ya kusaidia ya kuokoa maisha ya watu ambao wanauhitaji wa damu na wasipopata damu hiyo ni kuhataraisha maisha yao.
Milišić amesema licha ya kuchangia damu kuna umuhimuwa kila mmoja akahamasisha umuhimu wa kuchangia damu bila yakuwepo kwa siku ya uchangiaji damu.
“Kuna umuhimu wa kawaida wa kuhakikisha kwamba ubora wa damu na usalama wa damu unakwenda sambamba na uwezekano wa wachangiaji damu ili kuendana na uhitaji unapatikanaji wa damu kwa wakati pindi pale mgonwa anapoahitaji” alisema Milišić.
Mwakilishi wa Meneja wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Osca Mashawiya amesema kuwa malengo ya damu ni kufika asilimia 100 lakini damu inayopatikana ni asilimia 70.
Amesema kuwa katika kipindi hiki kumekuwa na mwamko katika suala uchangiaji damu kwa makundi mbalimbali kujitokeza katika uchangiaji damu huku akisisitiza Hospitali kutumia damu vizuri kwani kama mgonjwa anaweza kutumia bidhaa zingine kwa ajili ya kuongeza damu basi hakuna haja kutumi damu
No comments:
Post a Comment