Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Profesa Eleuther Mwageni kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).
Profesa Mwageni ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) na anachukua nafasi ya Profesa Esther Ishengoma ambaye amemaliza muda wake.
Uteuzi huo umeanza tarehe 7 mwezi huu.
Wakati huohuo Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Neema Mwita kuwa Mjumbe wa Baraza la Ushindani.
Dkt. Mwita anachukua nafasi ya Dkt. Theodora Mwenegoha ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment