Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Samia Suluhu Hassan akitembea kwenye mfano wa Reli ya Kisasa itakayojengwa
kutoka Mwanza hadi Isaka mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika sherehe
zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa
kuhusu ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha kutoka Mwanza hadi Isaka km 341
mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani
Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert
Gabriel Luhumbi, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho, Mkurugenzi
Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa pamoja na viongozi wengine wa Chama, Serikali na
Bunge, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha
kutoka Mwanza hadi Isaka km 341
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi
waliohudhuria sherehe za uwekaji wa Jiwe la Msingi jiwe la Msingi Ujenzi wa
Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Mwanza hadi
Isaka mkoani Shinyanga katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo
tarehe 14 Juni, 2021.Sehemu ya Wananchi waliohudhuria sherehe za
uwekaji wa jiwe la Msingi mradi huo mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR ambao utagharimu kiasi cha
Shilingi za Kitanzania Trilioni 3.1
Baadhi ya mawaziri na viongozi wengine wa taasisi
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi mradi huo mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR ambao utagharimu kiasi cha Shilingi za Kitanzania Trilioni 3.1. (PICHA NA IKULU).Msanii wa Singeli Barobaro akitumbuiza huku
viongozi mbalimbali wakimtunza katika Sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi
mradi huo mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR katika eneo la Fela mkoani
Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa Buhongwa mkoani Mwanza wakati
akiendelea na ziara yake mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.
Wananchi wa Mkuyuni na Butimba
wakimshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu
Hassan aliposimama eneo hilo kuwasalimu leo tarehe 14 Juni, 2021.
No comments:
Post a Comment