ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 19, 2021

RC Kafulila Apiga marufuku makampuni yaliyohujumu wakulima wa pamba Simiyu


Samirah Yusuph, Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David kafulila amezipiga marufuku kampuni mbili za ununuzi wa pamba ambazo ni Chesano na Birchard kununua pamba mkoani humo kwa madai ya kuhujumu mbegu za pamba zilizotolewa na Bodi ya pamba kwa ajili ya wakulima wa zao Hilo msimu wa kilimo wa 2020/2021.

Marufuku hiyo ameitoa leo Juni 18,2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari alipo kuwa akitoa msimamo na uelekeo wa kinachoendelea katika ununuzi wa zao la pamba.

Kafulila amesema kampuni hizo za uchakataji wa pamba na kukamua mafuta zinatuhumiwa kubadilisha matumizi ya mbegu za pamba zilizokuwa zinatolewa kwa ajili ya wakulima na kuzipeleka kiwandani kukamuliwa mafuta.

Mbegu hizo zimetolewa na Bodi ya pamba ili ziende kwa wakulima lakini chama Cha ushirika (Amcos) kilichoipokea mbegu hiyo ilizitoa kwa makampuni hayo ambapo zilikamatwa zikiwa zinasafirishwa.

"Bodi ya pamba inapotoa mbegu hizi kuna asilimia za fedha za mkulima anakatwa hivyo mbegu isipofika kwa mkulima anakatwa pesa ambayo hakupata mbegu hivyo anakuwa amehujumiwa na kudidimizwa".

Uzalishaji wa  pamba Mkoa wa Simiyu katika msimu wa 2021/2022 matarajio ni kuzalisha pamba Tani laki tano huku uzalishaji wa pamba msimu wa 2020/2021 ukiwa Tani  64,000 na msimu wa 2019/2020 Tani 66,000.

Aidha Kafulila amewaelekeza wanunuzi wa pamba kushiriki katika mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la pamba tangu katika maandalizi ya mashamba Hadi mavuno ili kuongeza kuongeza uzalishaji wenye tija katika zao Hilo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Chesano Peter Bahini amesema kuwa kesi hiyo ipo mahakamani hivyo kuiomba serikali kutoa leseni ya kuendelea kununua mikoa mingine wakati ambao mahakama ikiendelea na shauri hilo.

No comments: