Advertisements

Monday, June 21, 2021

Serikali yaagiza maafisa biashara kupungu urasimu kwenye utoji huduma


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wakati Tanzania ikiwa kwenye uchumi wa kati unaotegemea zaidi viwanda,serikali mkoani Njombe imewataka maofisa biashara kutanua wigo  wa kibiashara   pamoja na kuondoa urasimu wakati wa utoaji huduma katika jamii.

Kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe,mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri wakati wa kufunga mafunzo ya siku tano ya sheria ya leseni za biashara chini ya wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA) amesema ni muhimu maofisa biashara wote nchini kuondoa urasimu wa kufanya makadirio ya biashara kwa kuwakomoa wananchi pamoja na kuongeza wigo wa kutafuta fursa zaidi badala ya kujifungia ofisini.

“Mimi naomba tukajitafakari zaidi,hawa wanaoanzisha biashara tuwalee na tuwathamini pamoja na kuwaelimisha kwasababu biashara inahitaji zaidi elimu”alisema Ruth Msafiri

Awali afisa leseni kutoka BRELA  Bi,Saada Kilabula alisema wameendelea kufanya majadiliano ya sheria za biashara ili kuweka mazingira rafiki kwa kila anayefanya biashara kwa maslahi mapana ya uchumi wao na taifa kwa ujuml

“Katika kutekeleza majukumu mara nyingi kuna kuwa kuna mkanganyiko ndio maana tumeanzisha haya mafunzo kwa kuanzia kwenye hii kanda ili wote twende kwa pamoja na tutoke na lugha moja tunamshukuru Mungu kwa siku hizi tano tuliyoyafanya ni makubwa”alisema Saada Kilabula

Baada ya mafunzo hayo yaliyohusisha maofisa kutoka mikoa mitatu ya Njombe,Iringa na Ruvuma baadhi ya maofisa biashara akiwemo Cassim Mohamed kutoka Mafinga na Upendo Mwankemwa kutoka halmashauri ya mji wa Njombe wamesema wanaamini sheria na mafunzo waliyoyapata yatakwenda kuwasaidia katika kuwaelimisha wafanyabiashara kwani wengi wao wamekuwa wakikaidi kukata leseni kutokana na uelewa mdogo katika suala la kufuata sheria katika biashara zao.

No comments: