Meneja
wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wao kwenye maonyesho
ya Biashara Jijini Tanga leo
Meneja
wa Kituo cha Uwekezaji(TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda
kushoto akieleza masuala yanayohusu kituo cha Uwekezaji kwa Naibu Waziri
wa Viwanda na Biashara Mh. Exaud Kigahe (MB) alipotembelea Banda leo
kwenye eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea Maonyesho ya Biashara
ya 8
Meneja wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda kushoto akieleza masuala
yanayohusu kituo cha Uwekezaji kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Mh. Exaud Kigahe (MB) alipotembelea Banda leo kwenye eneo la Mwahako
Jijini Tanga kunakoendelea Maonyesho ya Biashara ya 8
Meneja
wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda
katikati akiwa na watumishi wengine wa kituo hicho wakitoa elimu kwa
mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alitembelea banda lao |
KITUO
cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda yaKaskazini kimeshiriki Maonesho ya
Kibiashara ya 8 jijini Tanga kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusiana na
masuala mbalimbali yanayohusu uwekezaji hapa nchini.
Maonesho
haya kibiashara ya 8 yameandaliwa na Chemba ya Biashara, Viwanda na
Kilimo (TCCIA) kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Mkoa na Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuanzia tarehe 28 Mei na
yanatarajiwa kuendelea hadi tarehe 6 Juni 2021 katika viwanja vya
Mwahako jijini Tanga.
Maonesho haya yamekuwa yakifanyik ajijini
Tanga kila mwaka yakiwa na lengo la kuhamasisha na kukuza biashara na
uwekezaji mkoani humo na mikoa jirani na hivyo kuthibitika kuwa miongoni
mwa maonesho yanayofanya vizuri katika kuhamasisha na kukuza biashara
na uwekezaji, ubunifu, masoko, kuonesha fursa za uwekezaji na kusaidia
ukuaji wa viwanda hapa nchini.
Akizungumza katika Banda la
Maonesho la TIC, Meneja wa Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda alisema
wamekuwa wakijitokeza kushiriki maonesho hayo katika kutekeleza Sheria
ya Uwekezaji Na. 26 Sehemuya 6 (g) ambayo inakitaka Kituo cha Uwekezaji
kufanya na kusaidia uwekezaji wa ndani kupitia shughuli mbalimbali za
uhamasishaji ambazo ni muhimu katika kuhamasisha na kuwezesha kuongezeka
kwa uwekezaji wa ndani.
Amesema Kituo cha Uwekezaji Kanda ya
Kaskazini kimetumia fursa hii kuelezea kwa umma majukumu mbalimbali
yanayotekelezwa na Kituo hicho na fursa za uwekezaji zilizopo katika
mikoa ya Kanda ya Kaskazini yaTanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Alizitaja
miongoni mwa fursa zilizopo katika mikoa hii kuwa ni pamoja na ujenzi
wa viwanda vya kuzalisha saruji, chokaa, madawa ya binadamu, madawa ya
kilimo na mifugo, viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo na yale ya
mifugo kama nyama na maziwa.
Fursa nyingine za uwekezaji zilizopo
katika mikoa hii ni pamoja huduma za utalii na ujenzi wa mahoteli ya
utalii kutokana kuwepo kwa vivutio vingi vya utalii kama vile hifadhi ya
mbuga zaSaadani, Mkomazi, Mlima Kilimanjaro, hifadhi ya mbuga ya
Arusha, Serengeti, Manyarana Ngorongoro.
Aidha, kuna fursa za
uwekezaji katika sekta ya kilimo, ujenzi wa majengo yabiashara,
usafirishaji, huduma za mashule na mahospitali, n.k.
Bw.Riganda
amesema katika kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali
zinazohusiana na uwekezaji kama vile cheti cha vivutio vya uwekezaji,
huduma za upatikanaji wa ardhi, vibali vya ukaazi, vibali vya kazi,
usajili wa makampuni ya biashara, ushauriwa kodi, masuala ya mazingira,
ukaguzi na utoaji wa cheti cha ubora wa bidhaa, n.k, Kituo hicho
kimewaleta maafisa mbalimbali kutoka katika taasisi na mamlaka za
serikali ambao wanatoa huduma zote hizo pale pale TIC Makao Makuu
kupitia huduma za mahala pamoja.
Upatikanaji wa huduma hizo umepunguza muda na gharama ambazo wawekezaji wangezipata kwa kuingia ofisi moja hadi nyingine.
Kituo
cha Uwekezaji Kanda ya Kaskazini kinatoa rai kwa wawekezaji wote wa
ndani na nje kuzitumia fursa za uwekezaji ipasavyo kwa ajili ya
maendeleo ya miradi yao na taifa kwa ujumla. Ofisi za Kituo cha
Uwekezaji Kanda ya Kaskazini zipo mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Maonesho
haya ya siku kumi yameweza kuvutia wafanyabiashara mbalimbali,
wawekezaji, wajasiriamali (wachini na wakati) na asasi zisizo za
kiserikali kutoka katika mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro na
Manyara.
Miongoni mwa wawekezaji waliosajiliwa na TIC
walioshiriki maonesho haya ya biashara jijini Tanga ni pamoja na Tanga
Cement PLC (wazalishaji wa saruji ya Simba), D.D. Ruhinda and Company
Ltd (wazalishaji wa bidhaa zinazotokana na nyuzi za mkonge), Mamujee
Products Limited (wazalishaji wa bidhaa za manukato), Harsho Group
kutoka Kilimanjaro, Pee Pee Tanzania Limited (wazalishaji wa aina
mbalimbali za mifuko ya kufungia bidhaa), makampuni ya uzalishaji wa
chokaa, n.k.
Aidha taasisi mbalimbali za serikali pia zimetumia
maonesho haya kuelezea huduma zao vikiwemo taasisi zinazotoa huduma
wezeshi kwa wawekezaji kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wakala wa
Usajili wa Makampuni hapa nchini (BRELA), Mamlaka ya Maendeleo ya
Biashara Tanzania (TANTRADE), Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Tanga,
TCRA, n.k. Kauli mbinu ya maonesho haya mwaka huu inasema “Kilimo kwa
Maendeleo ya Viwanda”.
Akizungumza namna walivyofaidika kupitia
huduma za TIC, Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Harsho yaliyopo
mkoani Kilimanjaro, Bw. Harold Shoo amesema wanajivunia sana kama
wawekezaji wa ndani kuwekeza kwenye viwanda hususan katika kuzalisha
vifungashio mbalimbali na vyakula vya mifugo.
Wanasem abila TIC wasingeweza kukuza mitaji yao, kuingiza mitambo ya viwanda, na kuajiri wataalam wa kigeni ambao wamefanikisha sana uwekezaji hao.
Hata
hivyo wamelalamikia ucheleweshaji wa maombi ya vibali vya wataalam
wakigeni ambao kwa namna moja au nyingine umekuwa ukiathiri maendeleo ya
miradi yao.
Kituo cha Uwekezaji kimekuwa kikishiriki
maonesho haya karibu kila mwaka ukitoa mwaka jana ambapo maonesho haya
hayakufanyika kutokana na kuwepo kwa tishio la ugonjwawa COVID-19.
Maonesho haya yamefunguliwa tarehe 31 Mei 2021 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Exaud Kigahe (MB).
No comments:
Post a Comment