Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Luhumbi (katikati) akizungumza wakati
alipokuwa akifungua Maadhimisho ya Juma la elimu kitaifa yanayofanyika
eneo la Shirati wilayani Rorya. kulia ni Mratibu wa Mtandao wa Elimu
Tanzania (TEN/MET), Bw. OcholaWayoga na Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Bw.
Simon Odunga (kushoto).
Mratibu
wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga (katikati)
akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la elimu
kitaifa yanayofanyika eneo la Shirati wilayani Rorya. Kushoto ni mgeni
rasmi wa maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Robert
Luhumbi.
Mkuu
wa Wilaya ya Rorya, Bw. Simon Odunga akizungumza kabla ya kumkaribisha
mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la elimu
kitaifa yanayofanyika eneo la Shirati wilayani Rorya.
Mratibu
wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga akisisitiza
jambo kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la elimu kitaifa
yanayofanyika eneo la Shirati wilayani Rorya.
Bendi
ya Shule ya Wasichana ya Kowak ikiongoza maandamano ya uzinduzi
Maadhimisho ya Juma la elimu kitaifa yanayofanyika eneo la Shirati
wilayani Rorya.
Bendi
ya Shule ya Wasichana ya Kowak ikitumbuiza kwenye maandamano ya
Maadhimisho ya Juma la elimu kitaifa yanayofanyika eneo la Shirati
wilayani Rorya.
Baadhi
ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Wilaya ya Rorya wakiwa na
mabango ya jumbe anuai kwenye maandamano ya uzinduzi Maadhimisho ya Juma
la elimu kitaifa yanayofanyika eneo la Shirati wilayani Rorya.
Sehemu
ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Wilaya ya Rorya wakiwa na
mabango ya jumbe anuai kwenye maandamano ya uzinduzi Maadhimisho ya Juma
la elimu kitaifa yanayofanyika eneo la Shirati wilayani Rorya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Luhumbi pamoja na viongozi meza kuu
wakitembelea banda la Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kwenye
Maadhimisho ya Juma la elimu kitaifa yanayofanyika eneo la Shirati
wilayani Rorya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Luhumbi pamoja na viongozi meza kuu
wakipata maelezo kutoka Meneja wa Programu, Nicodemus Shauri kutoka
TEN/MET (kushoto) alipotembelea banda la Mtandao wa Elimu Tanzania
kwenye Maadhimisho ya Juma la elimu kitaifa yanayofanyika wilayani
Rorya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Luhumbi (wa pili kushoto) akipokea
nyaraka za machapisho na vipeperushi vya Mtandao wa Elimu Tanzania
(TEN/MET), Toka kwa Mratibu wa Mtandao hu, Bw. Ochola Wayoga
alipotembelea banda hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Luhumbi pamoja na viongozi meza kuu
wakitembelea mabanda mbalimbali kwenye Maadhimisho ya Juma la elimu
kitaifa yanayofanyika eneo la Shirati wilayani Rorya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Luhumbi pamoja na viongozi meza kuu
wakitembelea mabanda mbalimbali kwenye Maadhimisho ya Juma la elimu
kitaifa yanayofanyika eneo la Shirati wilayani Rorya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Luhumbi pamoja na viongozi meza kuu
wakitembelea mabanda mbalimbali kwenye Maadhimisho ya Juma la elimu
kitaifa yanayofanyika eneo la Shirati wilayani Rorya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Luhumbi pamoja na viongozi meza kuu
wakiwa wamesimama kupiga makofi alipokuwa akipokea maandamano ya
washiriki kwenye Maadhimisho ya Juma la elimu kitaifa yanayofanyika eneo
la Shirati wilayani Rorya.
Sehemu
ya wanafunzi anuai wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya
Juma la elimu kitaifa yanayofanyika eneo la Shirati wilayani Rorya.
Na Mwandishi Wetu, Rorya
MKUU
wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Luhumbi amepongeza shughuli
zinazofanywa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kwa kushirikiana na
Serikali kuchochea mabadiliko ya elimu kiubora nchini Tanzania. Amesema
kwa kutambua mchango huo uongozi unatoa ofisi ambayo itatumiwa na wadau
wa elimu mkoani hapo ili kuwasogeza karibu na kufanya kazi kwa
kushirikiana zaidi.
Mhandisi Luhumbi ameyasema hayo alipokuwa
akizindua Maadhimisho ya Juma la elimu kitaifa yaliyofanyika leo
Wilayani Rorya, huku akikiri kuwa licha ya juhudi za Serikali katika
kuboresha elimu wadau wa elimu wanaumuhimu mkubwa kushirikiana na
Serikali kuboresha elimu yetu nchini.
"...Ni ukweli kwamba ili
nchi yoyote iweze kundelea inahitaji kuwaelimisha wananchi wake ili
wawezekupata maarifa ya kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Hivyo hapana budi ya kwamba mifumo ya elimu izingatie misingi ya usawa
na iwe jumuishi. Ili hili lifanikiwe ni lazima wadau wote wawajibike kwa
nafasi zao," alisema Mkuu wa Mkoa akihutubia wananchi na wadau wa elimu
walioshiriki maadhimisho hayo.
Aidha aliongeza kuwa ili nchi
yetu iendelee kuimarika zaidi katika uchumi wa kati hatuna budi kuwekeza
nguvu zetu kwa makusudi kabisa katika elimu, na rasilimali watu wenye
elimu bora ni injini ya kuleta mabadiliko chanya katika nchi.
Hata
hivyo, alisisitiza kuwa sehemu muhimu ya kuimarisha uwekezaji kwa ajili
ya elimu bora ni pamoja na kuimarisha elimu msingi yaani kuanzia
madarasa ya awali hadi sekondari.
Alibainisha kuwa serikali
haiwezi kwenda peke yake katika kusimamia suala hilo, bali ni lazima
iunganishe nguvu ili kupata mafanikio katika elimu na mchango wa
mashirika na wadau wa maendeleo unatambulika sana pamoja na wananchi.
Kwa
upande wake, Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw.
OcholaWayoga akizungumza katika maadhimisho hayo, alisema lengo kuu la
maadhimisho ni kuhamasisha juu ya malengo endelevu hasa lengo namba 4,
kuhakikisha utolewaji wa elimu bora na itakaomjengea mtoto maarifa na
ujuzi wa kupambana kimaisha na hasa mtoto wa kike ambaye jamii nyingi
zimekuwa zikimsahau na hivyo kuishia kuolewa akiwa bado na umri mdogo.
Malengo
mengine ni pamoja na kuongeza uelewa kwa umma juu ya madai ya haki ya
elimu iliyo bora na kuhamasisha elimu kwa makundi maalumu kama vile
watoto wenye ulemavu. Alisema miongoni mwa shughuli zitakazo fanyika
baada ya ufunguzi ni kuwa na mikutano itakayofanyika vijiji mbalimbali
na wananchi Juni Mosi na Pili kuwahamasisha wanajamii kushirikiana na
Serikali katika kuboresha elimu iliyo jumuishi.
Hata hivyo
aliongeza kuwa lengo lingine la maadhimisho hayo ni kuhamasisha jamii,
Serikali na mashirika yasiyo na kiserikali umuhimu wa uwajibikaji wa
pamoja katika masuala ya elimu na utekelezaji wa lengo la maendeleo
endelevu la nne na hasa kuimarisha mifumo ikiwemo ya kuwekeza katika
TEHAMA.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni; Uwekezaji
katika mifumo ya Elimu kwa malengo ya maendeleo endelevu (Financing
Education System for Sustainable Development Goals), kauli
inayoikumbusha jamii umuhimu wa juhudi ya pamoja kama wadau wa elimu,
yaani serikali, Asasi za Kiraia, sekta binafsi, wanafunzi, wazazi na
wananchi kwa ujumla.
Burudani mbalimbali zikitolewa na wanafunzi kwenye maadhimisho hayo.
Mwenyekiti
wa Halmshauri ya Rorya, Gerald Ng'ong'a (wa tatu kulia) akitembelea
Banda la Haki elimu kwenye Maadhimisho ya Juma la elimu kitaifa
yaliyofanyika Wilayani Rorya.
Mwenyekiti
wa Halmshauri ya Rorya, Gerald Ng'ong'a (katikati) akitoa hela kununua
moja ya bidhaa zinazoandaliwa na taasisi ya Shule Direct alipotembelea
Banda hilo kwenye Maadhimisho ya Juma la elimu kitaifa yaliyofanyika
Wilayani Rorya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Luhumbi pamoja na viongozi meza kuu
wakitembelea banda la CAMFED kwenye Maadhimisho ya Juma la elimu kitaifa
yanayofanyika eneo la Shirati wilayani Rorya.
No comments:
Post a Comment