Advertisements

Monday, June 14, 2021

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aondolewa madarakani

 Benjamin Netanyahu amepoteza utawala wake wa miaka 12 madarakani nchini Israel baada ya bunge la taifa hilo kupiga kura ya kuidhinisha serikali mpya ya muungano.

Kiongozi wa mrengo wa kulia Naftali Bennett ameapishwa kuwa waziri mkuu akiongoza 'serikali ya mageuzi'.

Ataongoza muungano wa vyama ulioidhinishwa kupitia uongozi mwembamba wa walio wengi wa 60-59.

Bennett atakuwa waziri mkuu hadi mwezi Septemba 2023 ikiwa ni maafikiano ya ugavi wa mamlaka.

Baadaye atamkabidhi Yair Lapid - kiongozi wa chama cha mrengo wa kati cha Yesh Atid, kuongoza kwa miaka mingine miwili.

Netanyahu - kiongozi aliyeongoza kwa muda mrefu ambaye ametawala siasa za taifa hilo kwa miaka kadhaa atasalia kuwa kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia cha Likud na kuwa kiongozi wa upinzani.

Wakati wa mjadala katika bunge la Knesset , bwana Netanyahu ambaye hakukubali kushindwa aliahidi: ''Tutarudi''.

Baada ya kura hiyo kupigwa , Netanyahu alisimama na kumkaribia  Bennett kabla ya kumuamkia kwa mkono.
 

CHANZO -BBC

No comments: