Advertisements

Sunday, June 20, 2021

Wizara yatoa tahadhari wimbi la tatu la Ugonjwa wa Corona

Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kuwakumbusha tena na kuwatahadharisha wananchi wote Tanzania kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID-19. 
 
Tahadhari hii ya leo inatokana na hali ya mwenendo wa ugonjwa huu duniani na ongezeko la maambukizi katika nchi za Afrika zikiwemo nchi jirani zinazotuzunguka ambazo zimekumbwa na wimbi la tatu la mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 ambapo maambukizi yameendelea kuongezeka maradufu kuliko ilivyokuwa katika wimbi la pili. Hivyo wizara inawakumbusha wananchi wotekutopuuza ugonjwa huu wa COVID-19.

Ndugu wanahabari,

Wizara imeanza kuona viashiria vya kutokea kwa wimbi la tatu la mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 katika nchi yetu. Hii ni Kutokana taarifa za ufuatiliaji wa mwenendo wa ugonjwa huu zinazofanywa

na wizara na mwingiliano wa watu wetu na watu wa mataifa jirani na mengine duniani katika shughuli za kijamii na kiuchumi.

Ndugu wanahabari,

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani, inayotolewa katika jarida la wiki ya 24 inayoanzia tarehe 7 hadi 13 Juni 2021, katika kanda ya Afrika, idadi ya wagonjwa wa COVID-19 imekuwa ikiongezeka kwa wiki tano mfululizo mfano katika wiki moja iliyopita nchi za Afrika Kusini, Uganda, Zambia, Namibia, DRC, Angola na nyinginezo zimeendelea kuonyesha kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa isiyoshuka huku ikiripotiwa nchi hizo kukumbwa na anuai ya virusi vipya ambavyo vinasababisha ugonjwa wa COVID-19 kuwa mkali zaidi na pia kuathiri hata watu wenye umri

Ndugu wanahabari;

Jukumu la kinga dhidi ya ugonjwa huu ni la kila mmoja wetu, hivyo tusiwe na hofu ila tuendelee kuzingatia afua za kinga Hivyo, Wizara inawataka Viongozi wote wa serikali ngazi zote, sekta binafsi, Viongozi wa Kijamii na madhehebu ya dini kuwajulisha wananchi wote kuchukua tahadhari zote muhimu, kuelimisha, na kutekeleza afua za kujikinga na tishio la wimbi la tatu la mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19.

Ndugu wanahabari; Kama tunavyofahamu, Kamati Maalum iliyoundwa na Mh. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 

ilishauri hatua madhubuti ziendelee kuchukuliwa ambapo pia ilielezea kufuatilia kwa karibu viashiria vya kutokea kwa wimbi la tatu la ugonjwa wa COVID-19 nchini. Napenda kuwajulisha kuwa serikali imeendelea kufanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati na hivi karibuni mtajulishwa hatua za utekelezaji wake.

Hivyo napenda kuwakumbusha na kuwasisitiza wananchi wote kutekeleza yafuatayo katika kujikinga na ugonjwa wa COVID-19;

  1. kuendeleza tabia ya kunawa mikono mara kwa mara kwa maji safi tiririka na sabuni maeneo yote na iwapo maji tiririka na sabuni hakuna, basi tutumie vipukusi (sanitizer) katika maeneo yote
  1. Uvaaji wa barakoa safi na salama, ambayo umetengeneza mwenyewe au umenunua kwa watengenezaji wa ndani ya nchi yetu, waliothibitishwa na niwaombe watalam wa afya kutoa elimu juu ya uvaaji sahihi wa barakoa. Barakoa zivaliwe katika maeneo yote yenye msongamano wa watu.
  1. Kuepuka misongamano isiyo ya lazima ikiwemo kwenye vyombo vya usafiri, kwenye misiba, makanisani, kwenye mipira na hivyo kuzingatia kukaa umbali wa mita moja au zaidi kutoka mtu mmoja na mwingine na kuhakikisha maeneo hayo yanakuwa na mzunguko wa hewa wa kutosha
  1. Kufanya mazoezi mara kwa mara, kulingana na hali ya afya ya mtu, na mazingira aliyonayo, kama vile kutembea kwa kasi, si chini ya dakika 30 au zaidi, hadi kutoka jasho, kuruka kamba, kukimbia mwendo unaoona unakufaa na kufanya zoezi popote ulipo.
  1. Kuzingatia lishe bora inayojumuisha matunda na mboga za majani zinazopatikana nchini kwa gharama nafuu, kulingana na mazingira ya vyakula vya asili katika eneo analoishi mtu.
  1. Kwa wale wenye umri mkubwa, wenye uzito uliopitiliza na wenye magonjwa sugu kama Pumu, Shinikizo la juu la Damu, Kisukari, Magonjwa ya Moyo na Figo kuchukua hatua madhubuti
  1. Kuwahi matibabu kwenye vituo cha kutolea huduma za afya, mara waonapo dalili za ugonjwa wa UVIKO-19 kama Mafua Makali, Maumivu ya koo, Maumivu ya kichwa, Uchovu wa Mwili, Kupumua kwa shida, Kukosa Hamu ya Kula na

Kupoteza uwezo wa Kunusa harufu mbalimbali.

Ndugu wanahabari;

Wizara inapenda kuwakumbusha tena Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Viongozi wa wizara zote, Wakuu wa taasisi za umma na binafsi, Viongozi wote wa dini na kijamii kuchukua hatua za kiuongozi katika kuelimisha, kuratibu na kusimamia jamii katika kuchukua tahadhari. Aidha, wizara inawataka Waganga wakuu wa Mikoa na

Halmashauri na Maafisa Afya wanaotoa huduma mipakani kuendelea kuimarisha udhibiti wa magonjwa katika maeneo hayo kwa mujibu wa miongozo husika. Pia, kuendelea kufuatilia magonjwa na matukio hatarishi kwa afya kwenye maeneo yao, ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa Umma kuhusu namna ya kujikinga. Vilevile inawasisitiza kuratibu kwa karibu taarifa zote za magonjwa ya milipuko pamoja na magonjwa mengine mbalimbali na kutoa taarifa hizo kupitia mfumo wa ufuatiliaji mwenendo wa magonjwa nchini.

Mwisho Wizara inawakumbusha wananchi kuendelea kutoa taarifa zozote za kiafya na kupata ufafanuzi wa masuala ya kiafya na magonjwa ya mlipuko kupitia namba ya simu 199 bila malipo yoyote na kuwasihi wananchi kufuatilia na kuzingatia taarifa za mwenendo wa ugonjwa huu kutoka vyanzo rasmi vya serikali.

Asanteni sana

Imetolewa na

Mkurugenzi wa Kinga

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

No comments: