ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 22, 2021

Ligi Kuu Bara 2021/22 kuanza septemba

 


ZIKIWA zimepita siku chache baada ya msimu wa Ligi Kuu Bara 2020/21 kumalizika, imebainika kwamba msimu ujao wa 2021/22 unatarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi mwezi Septemba mwaka huu.

Ligi Kuu Bara ilifikia tamati Jumapili iliyopita, ambapo michezo tisa ya timu zote 18 ilipigwa, na kushuhudia klabu ya Simba ikikabidhiwa ubingwa wa nne mfululizo huku klabu za JKT Tanzania, Gwambina, Ihefu na Mwadui zikishuka daraja.

Kupitia ligi ya msimu huu, klabu nne zimefanikiwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao ambapo, Simba na Yanga zitashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Azam na Biashara United zikishiriki michuano ya kombe la Shirikisho.

Akizungumzia ratiba hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Almas Kasongo, amesema: “Msimu wa Ligi Kuu Bara tunatarajia uanze mwezi Septemba mwaka huu, ingawa mpaka sasa bado hatujapanga tarehe rasmi ya kuanza kwa ligi.

Wakati ligi ikitarajiwa kuanza mwezi Septemba, juzi Jumatatu, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilitangaza kufunguliwa rasmi kwa dirisha la usajili ambalo litafungwa Agosti 31, mwaka huu.

No comments: