Mchungaji Ambilikile Mwasapile maarufu kwa jina la 'Babu wa Loliondo', ambaye alipata umaarufu wa kutoa tiba ya kikombe kilichokuwa kinadaiwa kutibu magonjwa mbalimbali amefariki dunia.
Taarifa ambazo zimethibitishwa na mmoja wa waliokuwa wasaidizi wa mzee huyo, Paul Dudui zimesema mzee Mwasapile amefariki leo Ijumaa Julai 30, 2021 mchana katika kituo Cha Afya Cha Digodigo baada ya kuugua ghafla.
Dudui amesema mwili huo utapokelewa na viongozi wa Serikali wa Wilaya ambao ndio watatoa taarifa rasmi
No comments:
Post a Comment