Advertisements

Monday, September 13, 2021

WAZIRI BITEKO: MICHEZO NI AFYA TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA

Imeelezwa kuwa, michezo inaleta afya, akili , urafiki na kuwaweka pamoja Wafanyakazi wa Wizara pamoja na Taasisi zake.

Hayo yamebainisha leo Septemba 11, 2021 na Waziri wa Madini, Doto Biteko wakati wa ufunguzi wa Bonanza ya Wizara ya Madini na Tume ya Madini lililofanyika katika Viwanja vya Kilimani, Jijini Dodoma.

“Nawapongeza Wafanyakazi wote kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika michezo mbalimbali , tuendelee kufanya mazoezi ili tuweze kupata nguvu ya kuendelea kufanya kazi ya kulinda rasilimali zetu na kukuza Uchumi wa Nchi,” amesema Waziri Biteko.

“Nimechezesha vizuri mechi ya mpira wa miguu kama refa bila upendeleo wowote , niendele kuwapongeza wachezaji kwa kuwa mahiri na kucheza vizuri,” ameongeza Waziri Biteko.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amewapongeza washiriki wa Bonanza na kuwataka waendelee kufanya mazoezi mara kwa mara maana michezo ni furaha.

Naye, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba amesema Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan, anawasisitiza watu wafanyemazoezi kwa kuwa ni moja kati ya kinga ya kuufanya mwili kuwa imara ili kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

“Msisitizo kutoka kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ni kwamba Wizara na Taasisi zote za Serikali zifanye mazoezi kwa pamoja, na mazoezi hayo ni maandalizi ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) ambayo yamerudishwa na Serikali,”amesema Mhandisi Samamba ”.

Kwa upande wake, Kamishna wa Tume ya Madini, Janet Ruben amesema kuwa watu wapo ofisini lakin ukija kwenye mazoezi wapo, rai yangu tusiache mazoezi tushirikiane na kuwa pamoja Wizara na Tume ya Madini.

No comments: